HOME
WATU
zaidi ya 40 wanaodhaniwa kuwa majambazi, wameteka mabasi sita ya abiria
yanayofanya safari kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema atalitolea ufafanuzi leo.
Akizungumza na Gazeti la Mtanzania Kamanda Sabas, alisema mabasi hayo yalitekwa juzi saa 8 usiku, baada ya kufika eneo la Mbuga Nyeupe, Wilaya ya Longido, Mkoa wa Arusha.
Taarifa zilizopatikana jijini Arusha, zinasema baada ya majambazi hayo kuteka mabasi hayo yaliyokuwa yakitoka Nairobi kuelekea Arusha, waliwapora mali na fedha za abiria wote waliokuwamo.
Taarifa hizo, zinasema majambazi hayo yalifanikiwa kufanya uhalifu huo baada ya kuweka mawe barabarani, na baada ya kuyateka mabasi hayo, waliwaamuru abiria wote kushuka na kulala chini, huku wakipekuliwa na kutakiwa wasalimishe mali zote walizokuwa nazo.
Dereva wa moja ya mabasi yaliyotekwa, mali ya Kampuni ya Perfect Trans, Joseph John, aliwaambia waandishi wa habari kuwa majambazi hayo yalikuwa na silaha za jadi yakiwamo mapanga na mashoka.
“Kundi la majambazi lilikuwa kubwa, yaani walikuwa kama watu arobaini hivi, wametufanyia unyama wa kutisha kwa sababu wanawake walivuliwa nguo na vito vya thamani na wanaume tukivuliwa viatu na kuporwa kila kitu.. .Mimi ndiye nilikuwa dereva wa kwanza kufika na basi katika eneo hili, nilipoona mawe yamepangwa nilisimama ili kujua kilichokuwa kikiendelea na nilipojaribu kuyakwepa yale mawe, nilipigwa jiwe usoni hali iliyonifanya nishindwe kuendesha gari,”alisema dereva wa basi hilo.
Taarifa ya majambazi kuteka mabasi sita ya abiria Arusha na kuwadhalilisha kisha kuwaibia mali zao

Chapisha Maoni