HOME
Benki
ya NMB juzi January 25 ilikabidhi hundi ya Tshs mil. 75 kwa ajili ya
kudhamini mkutano wa mwaka wa maafisa wa Jeshi hilo yanayofanyika
Dodoma, leo kuna taarifa kwamba Benki hiyo imekabidhi pikipiki 5 aina ya
Honda kwa jeshi la polisi kwa ajili ya kusaidia kazi za kila siku za
jeshi hilo katika hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa St. Gasper katika
mkutano wa maafisa wa polisi unaoendelea Dodoma.
NMB imetoa msaada mwingine wa vitendea kazi kwa Jeshi la Polisi Tanzania

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Tom Borgols alikabidhi pikipiki hizo ambazo thamani yake ni Mil. 10 kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe.
“Tunashukuru sana kwa hizi pikipiki, zitatusaidia sana kuboresha utendaji wa polisi, tutaendelea kuwa wadau wenu muhimu” — Waziri Mathias Chikawe.
Team ya NMB ipo Dodoma
kwenye mkutano huo huku huduma mbalimbali za Benki hiyo zikitolewa
kwenye mabanda kadhaa ya maonyesho nje ya ukumbi wa St Gasper ambapo
unafanyika mkutano huo.

Kaimu CEO wa NMB, Tom Borgols akiwa na IGP Ernest Mangu pamoja na Meneja wa NMB Dodoma, Ole Loibanguti.




Mabanda ya NMB Wakala yaliyopo nje ya Ukumbi wa St. Gaspar Dodoma ambapo unafanyika mkutano huo.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Tom Boghols akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe ufunguo wa pikipiki ambazo NMB imezitoa kwa Jeshi hilo. Yupo pia Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa
Chapisha Maoni