HOME
Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Mikoani
Mkurugenzi
wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw. Raymond Mndolwa(aliyenyosha mkono juu)
akiekeza jambo wakati alipokuwa kwenye ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC
kwenye mradi wa nyumba za Makazi Wilayani Monduli jana.
Mkugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za makazi za kuuza zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo ya mradi wa
nyumba za kuuza za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli na
Msimamizi wa mradi huo Bw. Hassan Bendera.
Hii
ni sehemu ya nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kama
sehemu ya juhudi za Shirika hilo za kuwezesha wananchi wengi kumiliki
nyumba. Nyumba hizi zinajengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.
Msimamizi
wa mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli Bw.
Hassan Bendera (mwenye koti jekundu kushoto) akitoa maelezo kwa ujumbe
wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yanayohusu hatua za utekelezaji wa mradi wa
nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua mchoro wa ujenzi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha na kuhimiza Halmashauri
hiyo kukamilisha ulipiaji wa nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya
kukamilisha mradi huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha na kuhimiza Halmashauri
hiyo kukamilisha ulipiaji wa nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya
kukamilisha mradi huo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli (katikati), Twalib Mbasha
akiuonyesha ujumbe wa NHC eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga nyumba
ambalo alisema lina miundombinu yote muhimu ikiwemo umeme na maji.
Chapisha Maoni