HOME
TANGA
Baraka Mbolembole
Ikijiandaa na mchezo wa Jumapili (hatua ya nusu fainali) wa michuano ya kombe la FA dhidi ya mabingwa watetezi na vinara wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) Yanga SC, timu ya Coastal Union ya Tanga kupitia kwa msemaji wake Oscar Assenga imesema kwamba, game ya Jumapili hii itakuwa ngumu kwa kila upande lakini bado wanaendelea kufanya maandalizi kuelekea mchezo huo utakaopigwa katika uwanb wa Mkwakwani, Tanga.
Coastal ilikuwa timu ya kwanza msimu huu kuishinda Yanga msimu huu na hilo lilitokea katika mchezo wa raundi ya 17 katika ligi huku ukiwa mchezo wao wa marejeano katika ligi.
Magoli ya mlinzi wa pembeni, Miraj Adam na kiungo, Juma Mahadhi yaliwapa ushindi wa 2-0 ‘Wagosi wa Kaya’ ambao hadi sasa wanashikilia mkia katika VPL. Yanga ilitolewa katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Afrika itakwenda Tanga kwa lengo la kutaka kushinda mchezo huo na kutinga fainali.
“Mechi itakuwa ngumu kama fainali hivyo tutapambana ili kupata ushindi. Maandalizi yapo vizuri na dhamira Yetu ni kuiondosha Yanga kwenye FA ili tuingie fainali then tuchukue ubingwa. Majeruhi madogomadogo lakini hayawezi kuwakosesha mechi wachezaji na dhamira kubwa ni kumtumbua Yanga na si vinginevyo. Tunajua wameshatumbuliwa na waarabu sisi tutaendelea kutumbua maeneo mengine yaliyobakia.”, anasema kiongozi mmoja wa Coastal Union.

Chapisha Maoni