Title: MSHAHARA WA RAIS WA TANZANIA KWA MUJIBU WA KATIBA YA 1977
Author: Unknown
Rating 5 of 5
Des:
HOME DAR ES SALAAM Baada ya vuta nikuvute juu ya suala la mshahara anaolipwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pom...
HOME
DAR ES SALAAM
Baada
ya vuta nikuvute juu ya suala la mshahara anaolipwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, na kuibuka hadharani
kutaja kiasi anacholipwa ambacho ni shilingi milioni 9.5 kwa mwezi.
Mara baada ya Dk. Magufuli kuweka bayana
suala hilo kupitia Clouds 360 ya Clouds Televisheni, baadhi ya wabunge
wa upinzani waliibuka na kumtaka ataje posho mbali na mshahara
alioutaja.
Suala hilo limeibuliwa tena bungeni
mjini Dodoma baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Upendo Peneza (Chadema)
kumuomba Rais John Magufuli kujipunguzia mshahara.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 43 (1), inasema Rais
atalipwa mshahara na malipo mengineyo na atakapostaafu, atapokea malipo
ya uzeeni, kiinua mgongo, posho, kadiri itakavyoamuliwa na Bunge na
mshahara, malipo hayo mengineyo, malipo ya uzeeni na kiinua mgongo
hicho, vyote vitatokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya serikali na
vitatolewa kwa mujibu wa masharti ya ibara hiyo.
Ibara ndogo ya pili inasema mshahara
na malipo mengineyo yote ya Rais havitapunguzwa wakati Rais atakapokuwa
bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba.
Rais Magufuli alilazimika kutaja kiwango
cha mshahara anaopokea kufuatia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu (Chadema) na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),
kumpa changamoto ya kutaja mshahara wake, baada ya kueleza nia ya
serikali yake kupunguza mishahara ya watumishi wa mashirika na taasisi
zake kutoka Sh. milioni 40 hadi milioni 15.
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Chapisha Maoni