Unknown Unknown Author
Title: KENYATTA AWA – UNFOLLOW KIKWETE NA JACOB ZUMA KWENYE TWITTER
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME NAIROBI,KENYA MIONGONI watu maarufu hivi sasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashiriki katika mtandao wa kijamii wa Twitter ...
HOME

NAIROBI,KENYA


MIONGONI watu maarufu hivi sasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashiriki katika mtandao wa kijamii wa Twitter ni pamoja na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, hii ni kutokana na kuwa na wafuasi wengi ambao wanamfanya kuwa na jumla ya wafuasi milioni 1 akiwa nyuma ya Rais Paul Kagame wa Rwanda ambaye anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi.

 

Moja kati ya tukio ambalo limegonga vichwa vya habari katika mitandao ya kijamii hasa huo wa Twitter ni kitendo cha Kenyatta kuamua ku-unfollow  baadhi ya watu mashuhuri akiwemo Makamu wake wa Rais Willium Rutto pamoja na Mkewe Margaret Kenyatta.

 Wengine alio wa unfollow Rais Kenyatta ni msemaji wa Ikulu ya Kenya  Manoah Esipisu ,Mkurugenzi Mkuu wa Safaricom CEO Bob Collymore,Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya  Joseph Boinnet, Katibu Mkuu Kiongozi wa Kenya (CS) Eugene Wamalwa, Rais wa Afrika Kusini  Jacob Zuma na Rais wa zamani wa Tanzania  Dk. Jakaya Kikwete.

 

Pamoja na hayo,Kenyatta ameamua kusalia na watu 11 tu ambao ndio amewafollow kupitia ukurasa wake huo wa Twitter ,watu hao  ni pamoja na Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli, Rais wa Marekani Barrack Obama, Rais wa Ufaransa François Hollande ,Waziri Mkuu wa  India Narendra Modi na Waziri Mkuu wa Japan Abe Shinzo.

Miongoni mwa viongozi wengine wa Afrika waliosalia katika orodha ya watu 11 wa Kenyatta ni pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Nigeria  Muhammadu Buhari na Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika  Akinwumi A. Adesina.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top