HOME
Kikosi
cha timu ya Bunge ambacho kitashuka dimbani jioni ya leo kimejiandaa
vya kutosha kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo ambapo amebainisha kuwa,
wachezaji wake wote wameshaandaliwa kisaikolojia na kimchezo hivyo
wanatarajia ushindi wa kishindo. (Picha zote na Andrew Chale -Zanzibar) Wa Michuzi blog
Timu
ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge
Sports Club jioni ya leo kinatarajiwa kushuka dimbani kucheza mchezo
maalum na wa kwanza dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, mchezoutakaochezwa uwanja wa Amaan, Unguja.
Tayari
asubuhi ya leo kikosi hicho cha timu ya Bunge kimefanya mazoezi ya
mwisho kujiandaa na mchezo huo wa jioni ambao unatarajia kuchezwa majira
ya saa 12:45 Jioni katika uwanja wa Amaani. Kikosi hicho kinachonolewa
na Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa,
Mh. Venance Mwamotto amebainisha kuwa lengo la mchezo huo ni kiuimalisha
Muungano ambapo pia michezo ni afya hivyo mchezo utakuwa ni wa
ushindani na wa kuvutia kwa pande zote mbili.
“Tunawaomba
wabunge wote kutuunga mkono katika mchezo huu kwani tmu imejindaa vya
kutosha kuhakikisha tunashinda wetu huu wa leo Aprili 26 katika uwanja
wa Amaan karibuni watu wote kutushuhudia tutakavyoonyesha uwezo wa hali
ya juu katika michezo” alieleza Mh. Mwamotto.
Naye
Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Mh. Steven Ngonyani ‘Maji Marefu’
ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa timu hiyo ya Bunge amewaomba
wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapiga hatua kwani timu ni nzuri
na ina hali ya ushindi kwa pande zote hivyo anahakika na kuibuka na
ushindi kwa mchezo wa leo.
Kwa
upande wake Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi
Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge amewataka wabunge wote
wanaounda timu hiyo kuzingatia maelekezo ya Kocha pamoja na kuzingatia
taratibu za mchezo wa soka ilikuweza kupata ushindi mnono.
Kwa
upande wa Kapteni mpya wa timu hiyo, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda amesema kikosi cha timu yake
kimejiandaa vya kutosha na kiko kamili kwa mchezo huo wa jioni ya leo
huku akiahidi ushindi mkubwa.
Mchezo
huo wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya Muungano
wa Nchi ya Jamhuri ya Tanganyika Na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambapo
jioni ya leo viongozi mbalimbali watajumuika kushuhudia mchezo maalum.
Kikosi
cha Bunge chenye wachezaji zaidi ya 19 kimejiandaa vya kutosha katika
kuakikisha inapata ushindi mnono ambapo kimepiga kambi visiwni hapa kwa
siku kadhaa hivyo mchezo huo utakuwa ni wa ushindani kwa pande zote
mbili licha ya timu ya Baraza la Wawakilishi ambayo imejaa vijana wengi
yenyewe ikiwa imejificha katika kambi yao nje ya mji wa Unguja.
Aidha,
mbali na mchezo huo, pia kutakuwa na michezo mingine ikiwemo mchezo wa
Ligi ya Zanzibar pamoja na mchezo maalum ambapo Wekundu wa Msimbazi
Simba Sc ikitarajiwa kushuka dimbani kucheza na moja ya timu ya Visiwani
hapa mchezo ambao ni wa kirafiki katika kunogesha Muungano huo.
Kapteni
mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini,
Mh. Sixtus Mapunda akifanya mazoezi ya mwisho mwisho asubuhi ya leo
katika uwanja wa Amaan, Unguja
Chapisha Maoni