Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama Mh.Lembeli James Daudi
Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kahama kwa tiketi
ya (CHADEMA) Mh James Lembeli amemuomba Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania
Mh John Pombe Magufuli kwenda Kahama ili amuonyeshe majipu yalipo kwa lengo la
kuleta maendeleo katika halmashauri ya Mji wa Kahama.
Lembeli ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika mkutano wa Hadhara uliofanyika katika
viwanja vya CDT mjini Kahama uliolenga
kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Kahama kufuatia kumalizika kwa uchaguzi mkuu
na kesi yake dhidi ya Mbunge wa sasa Jumanne Kishimba.
Akiongea katika mkutano huo Lembeli amesema kuwa
halmshauri ya mji wa Kahama imejaa madudu mengi yanayosabaisha kasi ya
maendeleo kuwa ndogo huku akisema kuwa wanaosababisha madudu hayo wapo ndani ya
halmashauri na anawajua wote.
Kutokana na hali hiyo Lembeli amemuomba Rais Magufuli
kufika mjini Kahama ili amonyeshe majipu yalipo na ayatumbue na kuongeza kuwa
wanaoiharibu Tanzania wengi wao ni wale waliomzunguka Rais ambao ni majipu
makubwa yenye usaha mwingi wa Ufisadi.
Mbunge wa viti maalum Salome Makamba akihutubia halaiki ya wananchi waliohudhuria mkutano huo
Katika hatua nyingine Lembeli amekemea kitendo
kinachofanywa na baadhi ya maafisa mjini Kahama kwa kushirikiana na Mbunge wa
jimbo hilo Jumanne Kishimba kugawana eneo la Bwawa la Nyihogo ambalo husaidia
kutoa huduma ya maji kwa Hospitali ya wialaya ya Kahama na Gereza la Kahama.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA)
Salome Makamba amewahaidi wananchi wa Jimbo la Kahama kuwawakilisha vyema
Bungeni ikiwa ni pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya mji wa Kahama
kwa lengo la kutetea maslahi ya wananchi wa Kahama.
Mbunde wa Bukoba mjini Mh. Willfred Rwakatare akihutubia mkutano wa hadhara mjini Kahama
Naye Mbunge Mualikwa kutoka jimbo la Bukoba mjini
Willfred Lwakatale ambaye alikuwepo katika mkutano huo amewataka Viongozi wa
dini kuacha kuliombea taifa kinafiki na badala yake wakemee maovu ikiwezekana
kwa kuwataja mafisadi na wezi katika maombi yao ili kulinusuru taifa na watu
wachache wanaonufaika kupitia feha za umma wa Wawatanzania.
Chapisha Maoni