HOME
Watu
wawili wameuwa kwa kukatwa mapanga sehemu mbalimabli za miili yao
mkoani Geita akiwemo muuguzi wa Zahanati ya Kagu kwa kile kinachodaiwa
kuwa imani za kishirikina.
Tukio la kwanza limetokea juzi majira ya saa moja jioni ambapo Helena Paulo (56) mkazi wa kijiji cha Luhuma alikatwa mapanga wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake huku Elizabeth Masango (54) ambaye ni muuguzi wa Zahanati naye alikatwa mapanga akiwa nyumbani kwake.
Wakizungumza na Channel Ten baadhi ya mashuhuda wa matukio hayo wamesema vitendo vya uhalifu wa kukatwa mapanga akinamama vinaongezeka mkoani Geita, jambo linalowafanya kuishi kwa mashaka.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Ali Kidwaka aliyekwenda kutoa pole kijijini Kagu amewataka wananchi kuwafichua watu wanaofanya unyama huo huku mwenyekiti wa kijiji hicho Tanga Daudi amesisitiza ulinzi mkubwa wa jadi umeimarishwa kila kona.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo amesema mtu mmoja anashikiliwa kwa mahojiano kufuatia matukio hayo.

Chapisha Maoni