HOME
April 24 2016 ndio siku iliyokuwa
inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania, kwani ndio ile siku
ambayo ilikuwa inasubiriwa na mashabiki kushuhudia nusu fainali ya Kombe
la FA (Azam Sports Federation Cup), kwa upande wa Yanga walikuwa wageni
wa Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kutoka katika uwanja wa Mkwakwani Tanga
mechi imeshindwa kumalizika baada ya mashabiki wa Coastal Union
kutoridhishwa na uchezeshaji wa refa hivyo mchezo umeshindwa kuendelea
kutokana na kuwa na giza, kwani kumalizika kwa dakika 90 sare ya goli
1-1, kulifanya mchezo huende dakika 30 za nyongeza.
Chapisha Maoni