HOME
Kwa upande wa Azam FC walikuwa Shinyanga
katika uwanja wa Mwadui FC kucheza mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe
la FA (Azam Sports Federation Cup), Azam FC wapo katika uwanja ambao
inaaminika ni mgumu kwa mgeni kupata matokeo hususani katika mchezo
muhimu kama huu wa nusu fainali.
Mchezo ulianza kwa Azam FC kufunga goli
la kuongoza dakika ya 3 kupitia kwa Hamisi Mcha, goli ambalo
lilisawazishwa na Kabunda na kufanya dakika 90 zimalizike kwa sare ya
goli 1-1, mambo yalibadilika baada ya kuanza kwa dakika 30 za nyongeza
na Hamisi Mcha akapachika goli la pili kwa Azam FC lakini Jabir Aziz
akaisawazishia Mwadui FC dakika moja kabla ya dakika 120 za mchezo
kumalizika.
Hata hivyo mechi ililazimika kuamuliwa
kwa mikwaju ya penati na Azamf FC ikaibuka ushindi wa penati 5-3,
mikwaju ya penati ilipigwa baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya
goli 2-2.
Chapisha Maoni