Unknown Unknown Author
Title: UNAZIJUA SABABU ZA YANGA, AZAM KUAGA MASHINDANO YA KIMATAIFA?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Na Albogast Benjamin Ni safari ambayo imekuwa ngumu kwa abiria anayetokea Tanzania kuweza kufika eneo mahsusi, hakika safari hi...
HOME

Na Albogast Benjamin

YANGA NA AZAM

Ni safari ambayo imekuwa ngumu kwa abiria anayetokea Tanzania kuweza kufika eneo mahsusi, hakika safari hii ni ngumu kuliko safari zote japokuwa ni safari muhimu lakini kama imetushinda tuachane nayo. Tangu mwaka 2003 walipofanikiwa kuvuka safari hiyo abiria 11 kutoka Simba hadi leo hakuna abiria wengine walioweza kupenya kwenye safari hii.

Kwanini Timu za Tanzania zote zimeaga mashindano ya kimataifa?

Jibu ni moja tu safari hii inahitaji fedha ya kutosha kwaajili ya nauli na akiba ili uweze kufika unapopataka kwa bahati mbaya ni kwamba vilabu vyetu havihitaji kuwekeza kwaajili ya ushindi lakini wako tayari kuwekeza kwenye matangazo ya kuhamasisha mashabiki kwenda uwanjani, inasikitisha sana, Azam, Yanga, Simba nani amewaambia shabiki hatakuja kama mkicheza vizuri? Najua hakuna jibu.

Azam imewakosa Kapombe na Paschal Wawa kwenye benchi hakuna wachezaji wa aina yao je unategemea itashinda? Yanga wamecheza na Al Ahly 2014 wakatolewa wamekuja wamepiga kelele kwenye vyombo vya habari kuwa ni wakimataifa wamekwenda tena kukutana na wakimataifa wameonekana ni  wa Jangwani. Jifunzeni kutoka kwa timu iliyowatoa mara mbili ili siku nyingine na nyie muwatoe.

Nani alaumiwe?

Pengine siwezi kuwalaumu labda muda bado au safari ni ngumu kwasababu imemshinda mpaka Bingwa mtetezi Tp Mazembe lakini naamini wao wanajipanga kutokana na kuondokewa na wachezaji wao tegemeo kama Samatta ila Donald Ngoma peke yake hawezi kuwa Ronaldo pale Madrid ndio mana Tp Mazembe waliwachukua wachezaji wawili Samatta na Ulimwengu ili wawe na kikosi kipana na huo ndo uwekezaji wa safari iliyobora uhakika.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top