Unknown Unknown Author
Title: Yanga wameshindwa kulipa kisasi cha 2014 cha kuifunga Al Ahly ya Misri, wamekubali kipigo hiki
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Siku moja baada ya kutolewa kwa klabu ya Azam FC katika michuano ya Kombe la ...
HOME
Siku moja baada ya kutolewa kwa klabu ya Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na klabu ya Esperance ya Tunisia, macho ya watanzania April 20 2016 yalielekezwa katika mchezo kati ya Yanga wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Yanga ambao mchezo wa awali uliochezwa Taifa Dar es Salaam walimaliza kwa sare ya goli 1-1, walienda Misri katika mji wa Alexandria kutafuta sare ya goli 2-2 ili waweze kufuzu au washinde mchezo huo kwa bahati mbaya Yanga wamekubali kipigo cha goli 2-1.
Klabu ya Al Ahly ya Misri ndio walianza kupata goli la uongozi kipindi cha pili, lakini Yanga walisawazisha dakika ya 57 kupitia kwa Donald Ngoma aliyetumia vyema krosi ya Juma Abdul, mambo yalizidi kubadilika zaidi kuanzia dakika ya 80 baada ya Al Ahly kuongeza nguvu ya kuishambulia kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la ushindi dakika ya 95.
Kwa matokeo hayo Yanga wanakuwa wamerejea rekodi yao ya kufungwa na Al Ahly ya Misri, ambayo mwaka 2014 walifungwa tena katika hatua ya mikwaju ya penati 5-4 kwa nne. Yanga kwa sasa wanarudi kushiriki Kombe la shirikisho barani Afrika.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top