NEWSROOM NEWSROOM Author
Title: Airtel yatoa msaada wa Kompyuta 30 kwa chuo cha taifa cha utalii.
Author: NEWSROOM
Rating 5 of 5 Des:
HOME   Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi kompyuta 30 kwa Meneja Msaidizi wa chuo cha Taif...
HOME



  Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) akikabidhi kompyuta 30 kwa Meneja Msaidizi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)  Oscar Mwambene (katikati)   kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto) katika hafla iliyofanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
 Mkuu wa idara ya Utalii katika Chuo cha Taifa cha Utalii Elina Makanja (Kushoto) akimwelekeza mwanafunzi Agape Gerald (Kulia) mara baada ya kukabidhiwa kompyuta 30 kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Katikati)
Meneja wa huduma za jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (Kulia) akizungumza na vyombo vya habari wakati wa hafla ya makabidhiano ya kompyuta 30 kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa, akishuhudiwa na Meneja Msaidizi wa chuo Oscar Mwambene (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Mafunzo Eunice Nderingo Ulomi (kushoto), hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo Temeke, Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) wakitumia kompyuta zilizokabidhiwa na Airtel kwa kupitia mpango wa Airtel FURSA ili kuwawezesha kujifunza elimu ya ujasiriamali kwa njia ya kisasa.


Katika kuendeleza dhamira  yake ya kusaidia Jamii kwa kujenga ubora wa ya elimu ya ICT hapa nchini, Airtel imekabidhi kompyuta 30 kwa Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) ambapo ni sehemu mojawapo ya  mipango yake ya kusaidia vijana wajasiriamali hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA  wa kutoa huduma kwa jamii  katika kuboresha upatikanaji wa teknolojia ya kisasa na ubora wa elimu nchini Tanzania.

Kama kampuni yenye kutoa huduma bora za simu za mkononi, Airtel itaendelea kusaidia sekta ya ICT hapa nchini kwa kuwawezesha  vijana kupata elimu iliyobora  na kuwa vijana wenye mafanikio katika Jamii yao.

Akizungumza wakati wa sherehe za makabidhiano hayo  yaliyofanyika katika Chuo cha utalii cha Taifa (NCT) kilichopo Temeke, meneja huduma kwa jamii wa Airtel,  Hawa Bayumi alisema kuwa Airtel itaendeleza dhamira yake ya kuunga mkono juhudi ya kuboresha kiwango cha elimu hapa nchini.

“ Leo hii tumekabidhi kompyuta hizi tukiamini  kwamba tunachangia nchi yetu kuwa na elimu bora, ni jambo la muhimu kwa wanafunzi na walimu kuwa na vifaa bora mashuleni. Ndio maana Airtel imeweka mkazo katika swala la kusaidia Jamii kwa upande wa elimu  kwa kutoa vitendea kazi vitakavyoweza kusaidia kujifunzia na kupata elimu ya ujasiriamali na hatimaye kuchangia vyema na kupata matokeo bora. Kutokana na msaada huu kwa NCT tunaamini kabisa kwamba kiwango cha elimu kwa Wanafunzi kitaongezeka na hata urahisi wa walimu katika ufundishaji utaongezeka kwa kiwago kikubwa, na vile vile tunawawezesha kizazi kijacho kujikita zaidi katika teknolojia na kujua mambo mengi zaidi yanayoendelea dunia nzima kutokana na technolojia inayokuwa kila siku, "alisema Bayumi

Akizungumza kwa niaba ya chuo, mkurugenzi wa Mafunzo wa NCT, Eunice Nderingo Ulomi, aliwashukuru Airtel kwa kwa msaada huo wa kompyuta , na kubainisha kuwa kompyuta hizo zitachangia kuongeza kiwango cha elimu kwa mwanafunzi kitaaluma. "Mara nyingi kompyuta huwa inatazamwa kama si kitu cha muhimu katika Jamii yetu, ila ni kifaa muhimu sana kinachomuwezesha mwanafunzi kupata habari nyingi sana za masomo na hata kujua mambo mbalimbali yanayoendelea dunia nzima hasa katika karne hii ya 21," alisema Ulomi.

"Lengo letu ni kuhakikisha tunatoa elimu iliyobora katika  sekta ya utalii . Kupokea kompyuta hizi kutaboresha hali ngumu  tuliyakuwanayo ya upungufu wa vifaa hivi hapa chuoni na tunaamini tutatoa elimu iliyobora ambayo itasidia kupunguza changamoto tulizakuwanazo, ambazo zimekuwa zikitufanya tukwame katika mambo mengi sana, hivyo zitatusaidia  kukuza ujuzi wa kila mtu hapa chuoni, vile vile zitasaidia kuongeza mapato ya serikali, kukuza nchi yetu  katika ushindani wa kitalii na kuongeza uingizaji wa watalii ambapo itasaidia kuongeza sekta nyingine za kiuchumi katika upande wa maonyesho ", aliongeza Ulomi

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top