NEWSROOM NEWSROOM Author
Title: Naibu Spika Aahirisha Bunge Baada ya Wabunge Kumgomea Alipokataa Hoja ya Wanafunzi 7,000 Kutimuliwa UDOM
Author: NEWSROOM
Rating 5 of 5 Des:
HOME Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirisha shughuli zake za bunge leo majira ya saa tano asubuhi baada ya Mb...
HOME



Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirisha shughuli zake za bunge leo majira ya saa tano asubuhi baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) kuomba mwongozo na kutaka sakata la wanafunzi zaidi ya 7000 wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM waliokwama Dodoma baada ya kufukuzwa chuoni lijadiliwe. 


Baada ya Mhe.Nasari kuwasilisha hoja hiyo, naibu spika Dkt.Tulia Ackson Mwansasu, alikataa kujadiliwa kwa hoja hiyo hali iliyosababisha hali ya hewa kuchafuka bungeni.


Kauli ya naibu spika kukataa kujadiliwa kwa hoja hiyo, iliwanyanyua wabunge wa upinzani na baadhi ya wa CCM wakipinga kauli hiyo huku wakiwa wamesimama jambo ambalo lilisababisha kuaihirishwa kwa bunge hadi saa 10:00 jioni huku akiagiza kukutana kwa kamati ya uongozi ya Bunge

Naibu Spika Tulia Ackson ameamuru Wabunge kutolewa nje ya bunge baada ya baadhi ya Wabunge hao kusimama kupinga kitendo cha bunge kakataa kujadili suala la Serikali kuwataka wanafunzi wa UDOM kurudi kwao ndani ya saa 24 kufuatia mgomo wa Walimu unaoendelea kwa sasa.
AW1A0974
Baadhi ya wabunge wakionekana kujadili jambo
AW1A0973
AW1A0917
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia alivyosimama kuainzisha hoja hiyo
AW1A0956
Mbunge wa Arumeru Joshua Nassari akifafanua zaidi
AW1A0959
Baadhi ya wabunge wakitoka nje
AW1A0960
AW1A0987
AW1A0986
AW1A0984

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala, Ushauri n.k.?Basi Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp 0719565345

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top