HOME
Mei 11 2016 Bunge la 11 limeendelea Dodoma, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2016/2017
Akisoma hotuba hiyo Waziri Ummy Mwalimu amesema…>>>’Hadi
kufikia mwezi machi 2016 Wizara imekusanya jumla ya Shilingi
87,117,583,604 ikilinganishwa na makadirio ya Shilingi
122,998,941,500.00 yaliyoidhinishwa kwa mwaka 2015/2016’
‘Hii
ni asilimia 70.8 ya makadirio ya makusanyo ambayo yamevuka lengo
kutokana na usimamizi thabiti na matumizi ya TEHEMA. Katika mwaka
2016/2017 Wizara inatarajia kukusanya Shilingi 163,755,679,857.00’
‘Ili
kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza kazi zilizopangwa katika mwaka
2016/2017, naliomba Bunge likubali kuidhinisha makadirio ya makusanyo ya
Shilingi 166,138,358,857 kutoka katika mashirika na Taasisi zilizopo
chini ya Wizara yangu na vyanzo vya makao makuu’
‘Aidha
naomba Bunge likubali na kuidhinisha makadirio ya matumizi ya Wizara
pamoja na Taasisi zake yenye jumla ya Shilingi 845,112,920,056.00 kati
ya fedha hizo, Shilingi 317,752,653,00.00 ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na Shilingi 527,360,267,056.00 ni kwa ajili ya utekelezaji wa
miradi ya maendeleo’
Chapisha Maoni