HOME
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha kubwa la Burudani JEMBEKA FESTIVAL 2016. |
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi
Amewahakikishia Ulinzi na Usalama wakazi
wa jiji la Mwanza na Vitongoji vyake pamoja na wageni wote watakao hudhuria tamasha la Jembeka
festival 2016 linalotarajiwa kufanyika
Jumamosi hii ya tarehe 21 Mei 2016 katika kiwanja Cha CCM Kirumba kilichopo jijini Mwanza.
Kamanda Msangi ameyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na kuzungumza
na Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (Jembejembe) Alipomtembelea
kwa lengo la kumkaribisha kuwa
miongoni mwa wageni waalikwa katika
tamasha hilo la kipekee nchini Tanzania.
“Napenda kutoa wito kwa wakazi wa jiji la Mwanza,wageni
kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na nje ya Tanzania hili ni tamasha la
kipekee hapa mkoani kwetu hivyo napenda kuwaasa wananchi wote kufurahi na
kuhudhulia tamasha hilo kwa furaha pia
napenda kutoa rai kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjaji wa
amani”,Alisema Kamanda Msangi.
Kwa
upande wake Dr. Sebastian Ndege amemshukuru Kamanda Msangi kwa
ushirikiano aliouonesha tangu awali na hili la sasa kuhakikisha
anaimarisha ulinzi na usalama siku hiyo ya tamasha na kuahidi kutumia
vyombo vyake vya habari katika kulisaidia jeshi hilo kutoa elimu ya
ulinzi shirikishi.
“Nashukuru
sana kwa ushirikiano tunaoupata kutoka kwa Jeshi la polisi ngazi zote
kwani wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Mwanza inakuwa salama hivyo
mimi pamoja na timu yangu tunaahidi kusimama bega kwa bega na jeshi letu
kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake stahiki linapokuja suala
la ulinzi, usalama wa mtu mmoja mmoja na hata utoaji wa elimu kwa umma
kuhusu namna ya kuzuia uhalifu, ili Mwanza yetu iwe mahali salama"
Aidha
Kamanda Msangi ameahidi kuimarisha Ulinzi wa ndani na nje kwa maeneo
yote ya wilaya ya Ilemela ambako uwanja wa CCM Kirumba ndiko
unakopatikana na amewatoa hofu
Wananchi wote pamoja na wageni watakaohudhuria tamasha hilo kwa kuhofia
usalama. "Atakaye kuja kwa hila tutamdhibiti"
Tamasha la Jembeka festival 2016 mwaka huu litatumbuizwa na
msanii kutoka nchi ya Marekani Neyo anayetarajiwa kutua nchini kesho usiku.
Wakali wengine kutoka hapa nchini Tanzania akiwemo Diamond, Juma Nature, Ney wa Mitego, Maua
Sama, Ruby, Fid q, Mo Music, Baraka da prince, na wengine kibao, wanatarajiwa kumwaga mvua ya burudani siku hiyo.
JEMBEKA FESTIVAL linaloandaliwa
na Jembe ni Jembe Entertainment kupitia Jembe FM, hufanyika kila Mwaka
mkoani Mwanza na tamasha hilo kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu
sabini toka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr Sebastian Ndege (kulia) akisalimiana na Katibu wa Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu alipomtembelea ofisini kwake mapema leo kwa lengo la kumkaribisha kuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika tamasha hilo la kipekee nchini Tanzania. |
Aksante sana Gazeti la Mwananchi toka Mwananchi Communication kwa kutusaidia kufikisha taarifa mlango kwa mlango PAMOJA SANA. |
Jumamosi
hii, May 21,2016 itakuwa ni Jembeka Festival Msimu wa Pili. Utamu wa
Jembeka Festival unaanzia kwa Mkali Neyo kutoka nchini Marekani pamoja
na Mkali Diamond Platnumz kutoka Tanzania. Pia watakuwepo wasanii
wengine kibao.
Kumbuka
ni katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza kwa kiingilio cha
Shilingi 10,000, 50,000 na 100,000 so huu ni muda wa kununua tiketi
mwana wa kwetu.
Imedhaminiwa
na Vodacom Tanzania! Vodacom Kazi ni Kwako. Special Thanks FastJet, EF
Outdoor, Mwananchi Communications,Samsung, Ndege Insurance, Syscorp
Corporation, KK Security, JembeFm-JembeniJembe, Gsengo Blog, Binagi
Blog, Michuzi Blog, DjChokaMusic.com, Lakairo Hotel na wadau wengine.
Chapisha Maoni