HOME
0 Kimenuka!! CCM WATIBUANA,ALIYEMLIPUA LOWASSA NAYE ALIPULIWA VIBAYA,KISA MAJI YA ZIWA VICTORIA
Katibu mwenezi mkoa wa Shinyanga ndugu Emmanuel Mlimandago |
Siku
moja tu baada ya naibu waziri wa zamani wa maji nchini Anthony
Diallo,ambaye sasa ni mwenyekiti wa ccm mkoa Mwanza kudai kuwa dhana
inayojengwa kwamba mradi wa maji wa ziwa Victoria ulifanikishwa kwa
nguvu ya aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowassa,ni potofu na afadhali
angetajwa Diallo
Moja ya magazeti ya Tanzania Raia Mwema la tarehe 24-30 Septemba 2014,lilitoka na kichwa cha habari "Diallo: Lowassa Kaleta Maji? Bora Mimi",kauli hiyo imezua kizaa.
Leo
katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga
Emmanuel Mlimandago ameibuka na kumtaka mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Mwanza Dkt Antony Diallo kuacha kumtuhumu na kumtolea kashfa mbalimbali
zisizothibitika na kumvujia heshima waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa
likiwemo suala la maji ya ziwa Victoria kuyatoa Ihelele mpaka Shinyanga
na Kahama kwamba ni kazi yake badala ya Lowassa.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Mlimandago alisema mwenyekiti huyo wa CCM
mkoa wa Mwanza amekuwa akitumia magazeti,Tv na mitandao ya kijamii
kumchafua mbunge wa Monduli Edward Lowassa kitendo alichosema kinatokana
na Diallo kutumika na mahasimu wa kisiasa wa Edward Lowassa.
Alisema
hata suala la maji ya ziwa Victoria kuyatoa Ihelele mpaka Shinyanga na
Kahama kama anavyodai yeye Diallo kuwa ni kazi yake aliyoifanya kipindi
akiwa naibu waziri wa wizara ya Maji,chini ya waziri wa wizara hiyo
wakati huo ikiongozwa na Lowassa,ni kuudanganya umma, kwani naibu waziri
hana uwezo huo.
“Mimi
kama mtanzania na kama kiongozi wa ChamaTumechoka kumvumilia,leo
namuonya aache,maneno aliyoyasema ni dhahiri kuwa ameonesha udhaifu wa
hali ya juu sana na hasa msomi kama yeye mwenye elimu ya
PHD,amewadhalilisha wasomi kwani naibu waziri huwa ana madaraka pasipo
mamlaka,namuomba aache kudanganya na kupotosha umma”,alisema Mlimandago.
“Watanzania
wanajua naibu waziri haiingii kwenye baraza la mawaziri labda iwe
leo,na tunajua naibu waziri hupangiwa kazi na waziri wake mwenye dhamana
ya wizara na hata bungeni hujibu maswali kwa niaba ya waziri,sasa
tunashangaa huo uwezo naibu waziri Diallo aliupata wapi,wakati alikuwa
chini ya waziri Lowassa?”,alihoji Mlimandago.
Aidha
alimtaka Diallo kuacha,chuki binafsi,fitina,majungu,siasa za majitaka,
uongo na upotoshaji na kutaka kujitafutia umaarufu na heshima
asizostahili kupitia mgongo wa Mheshimiwa Edward Lowassa.
“Diallo
amechelewa kuyazungumzia maji ya Ziwa Victoria kwani Wana Kahama na
Shinyanga wote kwa ujumla,wanajua kazi nzuri ya kupatiwa maji imefanywa
na aliyekuwa waziri mwenye dhamana ya wizara ya maji Mheshimiwa Edward
Lowassa”,aliongeza.
Katika
hatua nyingine alimtaka kuacha kuudhihirishia umma wa Watanzania kuwa
kumbe anatumika kuchamfua Lowassa huku akimwomba ayaseme mapungufu yake
kama vile kueleza kwanini wananchi wa jimbo la Ilemela waliacha
kumchagua nafasi ya ubunge mwaka 2010 na aleezee elimu yake na PHD
alivyoipata.
“Tunaomba
auleze umma,kitu gani kilimfanya aukose ubunge mwaka 2010,na ni kwa
kiasi gani alichangia na kusababisha jimbo la Nyamagana na kuanguka kwa
Mheshimiwa Laurence Masha na jimbo kuchukuliwa na upinzani kutokana na
siasa zake za chuki na visasi na kuendeleza siasa za bora tukose
wote”,alifafanua Mlimandago.
Katika
hatua nyingine alimshauri mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mwanza kutumia
muda wake kushughulika na kupanga mikakati wa jinsi ya kupambana na
mauaji ya akina mama vikongwe na albino ikizingatiwa kuwa mkoa huo
unaongoza kwa mauaji hayo nchini.
Aliongeza
kuwa ni vyema sasa Diallo akajikita kushughulika kuokoa majimbo yake
yaliyochukuliwa na upinzani mfano jimbo la Ilemela,Nyamagana na Ukerewe
kuliko kuendeleza malumbano na kugombania nafasi zisizokuwa na tija na
kwamba kutokana na kuwa yeye ni kiongozi wa chama apeleke hoja zake
kwenye vikao vya chama badala ya kuzungumza nje ya vikao
Chapisha Maoni