WAKATI serikali ikiwa katika utekelezaji
wa mpango wa matokeo makubwa sasa, hali imeonekana kuwa tofauti katika
shule ya sekondari Mwantini iliyopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
mkoa wa Shinyanga baada ya kukutwa na waandishi wa habari wakifyatua
matofali ya shule
majira ya saa 5:00
asubuhi muda ambao wangetakiwa kuwa darasani wakiendelea na vipindi vya
masomo. Wanafunzi hao wamekuwa wakifanya kazi hiyo wiki nzima bila
kuingia darasani huku wakikosa masomo ambayo ni haki yao ya msingi.
Katika mahojiano na waandishi wa habari wanafunzi hao walisema
wanasikitishwa na kitendo cha walimu kuwafanyisha kazi hiyo muda wa
masomo wakati wengine wanajiandaa kuanza mitihani ya kidato cha pili na
cha nne jambo ambalo linaweza kusababisha kiwango cha taaluma kushuka na
kushindwa kufikia malengo ya matokeo makubwa sasa(BIG RESULTS NOW
BRN).
Wanafunzi wakiendelea na kazi ya kuchanganya mchanga kwa ajili ya kazi ya kufyatua matofali.
|
Chapisha Maoni