Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Scotland yaendelea kuwa sehemu ya Uingereza Wapiga kura wa Scotland wamepinga katika kura ya maoni ya kihistoria wazo la kuwa huru...

Image

Scotland yaendelea kuwa sehemu ya Uingereza
Uamuzi wao umeunusuru usivunjike muungano mkongwe wa miaka 307 pamoja na Uingereza na kupelekea jamii yote tangu ya kisiasa mpaka ya kiuchumi kuteremsha pumzi.
Mshikabendera wa kambi ya "La" Alistair Darling anasema:"wamemechagua Umoja badala ya mtengano na mageeuzi ya maana badala kutengana kusikokuwa na maana...."
Waziri mkuu wa Uingereza,ambae tangu mwanzo amedhihirisha anaelemea upande wa kura ya "La"-hakuficha furaha yake alipotamka"Sasa tunabidi tuangalie mbele ,tusijali nani kapiga kura aupande gani,tushirikiane,katika kuijenga bora zaidi na kuipatia mustakbal mwema zaidi Uingereza yetu.Nakushukuruni na kukutakieni asubuhi njema."

Alex Salmond ataka ahadi zitekelezwe

Waziri mkuu wa Scotland,Alex Salmond ,mshika bendera wa kambi ya "Ndio" baada ya kukiri kambi yake imeshindwa amemtaka waziri mkuu wa Uingereza David Cameron,washirika wake wa Liberal Democratic na upande wa upinzani wa Labour watekeleze ahadi walizotoa za kuipatia madaraka makubwa zaidi Scotland.
Nje ya Uingereza spika wa bunge la Ulaya Martin Schulz alikuwa wa mwanzo kutoa maoni yake kuhusu kura ya maoni ya Scotland aliposema katika mitambo ya Radio moja ya Ujerumani "Naungama nimefurahishwa na matokeo ya kura ya maoni." Nitakapokutana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron nitamhakikishia "napenda kuiona Uingereza ndani ya Ulaya iliyoungana."Mwisho wa kumnukuu spika huyo wa bunge la Ulaya.

Hata masoko ya hisa yanashangiria

Faharasa katika soko la hisa la mjini London zimepanda kufuatia matokeo ya kura ya maoni ya Scotland.Hali hiyo ilianza tangu jana pale thamani ya sarafu ya Uingereza Pound ilipopanda kuiwango cha juu kuwa kushuhudiwa tangu miaka miwili iliyopita,dhidi ya sarafu ya umoja wa ulaya Euro.
Katika masoko ya hisa mijini Paris na Frankfurt,hali ni ya kutia moyo pia.CAC 40 ya Ufaransa imejipatia pointi 4.490.60 leo asubuhi huku DAX ya Ujerumani ikijipatia asili mia 0.54.
Waingreza sasa wanasubiri kitakachosemwa leo mchana na malkia Elisabeth wa pili anaekutikana katika kasri lake la balmoral kaskazini mashariki ya Scotland.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top