HOME
WANACHAMA
wa Tanzania Labour Party (TLP), wamemjia juu Mwenyekiti wao, Augustino
Mrema, kwa madai anang’ang’ania madaraka huku akishindwa kuitisha
uchaguzi mkuu kama katiba yao inavyoeleza.
Kutokana na hali hiyo, wanachama hao wakiongozwa na James Haule, wamemuandikia Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kuelezea kusikitishwa kwao na ofisi yake kukaa kimya juu ya hali hiyo.
Katika barua yao kwenda kwa msajili isiyokuwa na namba ya kumbukumbu ya Septemba 15 mwaka huu, wanachama hao wameeleza kuwa uchaguzi wa TLP ulipaswa kufanyika Januari 31 mwaka huu na kwamba, kuanzia siku hiyo mwenyekiti wao alipoteza sifa ya kuwa kiongozi.
Ilieleza, Wanachama wa TLP wanayo heshima kubwa ya kuandika barua hiyo kwa matumaini ya kupata ufumbuzi wa ukiukwaji wa katiba ya chama chao, ikiwa ni pamoja na sheria za nchi zinazowaongoza katika kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.
“Kutokana na kukiukwa kwa katiba… sisi wanachama tunaitaka ofisi yako kutoa mwongozo juu ya uitishwaji wa mkutano mkuu wa Chama kuanzia ngazi ya matawi hadi Taifa, kwa kuwa Chama sasa hakina viongozi, kwani waliopo sasa wamekosa sifa kuanzia Januari 31 mwaka huu,” ilisema barua hiyo.
Kwa upande wake, Mrema ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alipulizwa juu ya ukiukwaji wa katiba ya chama chake na kwamba hawako madarakani kwa mujibu wa katiba yao, alisema hawezi kujiongezea muda wa kuongoza bila kuungwa mkono na Katiba iliyopo.
Alisema anachojua kufanya jambo lolote kinyume na taratibu za kisheria ni kosa na kwamba, hawezi kuingia katika mtego huo.
“Mimi si mwendawazimu, nataka nikwambie misingi na kanuni iliyoniweka madarakani mpaka muda huu, lakini kwanza nipe dakika tano niwasiliane na wenzangu,” alisema Mrema.
Hata hivyo, baada ya kupigiwa simu katika muda aliyotoa, bado hakuwa na jibu la uhakika juu ya kipengele kinachompa fursa ya kuendelea kuwa madarakani huku akimtaka mwandishi aendelee kuvuta subira.
Hatua ya wanachama wa TLP kumkataa Mwenyekiti wao, ni muendelezo wa misukosuko inayompata kiongozi huyo katika uwanja wa siasa, baada ya hivi karibuni kukaririwa akimuomba Rais Kikwete amuondoe James Mbatia katika nafasi ya Ubunge ili asiweze kumpokonya Jimbo la Vunjo.
Wanachama TLP walia na Mrema

Chapisha Maoni