HOME
April 25
2016 imetolewa taarifa kutoka Ikulu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi John Kijazi ambayo imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.
Kamishna
wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius
Makuru Nyambacha ambaye amestaafu. Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa
Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi, uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo
tarehe 25 Aprili, 2016.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.
Chapisha Maoni