HOME
April 25
2016 Chama cha ACT Wazalendo kimekutana katika Mkutano wa Halmashauri
Kuu ya Chama jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake Kiongozi Mkuu wa
chama hicho Zitto Kabwe amempongeza Rais Magufuli kwa kuanza katika eneo moja muhimu sana ambalo anasema ni msingi mkubwa wa kuanzishwa chama chao.
Amelitaja
eneo hilo kuwa ni la kupambana na ufisadi, licha ya kumuunga mkono kwa
hatua hizo anazozichukua lakini amesema bado Rais hafanyi inavyopaswa na
hapa ameainisha vitu ambayo Rais hajavigusa kabisa ..
>>>’Kuna mambo ya muda
mrefu ambayo tunaendelea kama nchi kuyalipia Rais ameyakalia kimya mfano
suala la tegeta Escrow, bado mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na
kila mwezi serikali inawalipa matapeli hawa zaidi ya bil 8 wazalishe au
wasizalishe umeme, hivi ndio vikundi maslahi katika sekta ya nishati
ambavyo bila kuvibomoa Rais ataonekana anachagua katika vita hii‘.
>>>’Suala
la hatifungani la zaidi trilioni 1.2 ambazo serikali yetu ilikopa
kutoka benki ya Uingereza ni sawa kuwa kuna hatua tayari zimechukuliwa
lakini Serikali imefikisha mahakamani ni wanaoitwa madalali wa rushwa
hiyo, sio walioitoa wala walioipokea, hatifungani hii imeongeza deni la Taifa kwa kiwango cha trilioni 1.2 bila ya riba’.
>>>’Tungetarajia Rais
angewaongoza watanzania kukataa aina hii ya mikopo, lakini Takukuru
wanaona ni sifa kuweka ndani watu wa dola mil 6 na kutusaulisha kabisa
kwamba mkopo huu ambao kimsingi haupaswi kulipwa, ni wa trilioni 1.2 kwa
hiyo katika vita dhidi ya rushwa sio swala la kutumbua majipu tu ni
suala la kuweka mfumo madhubuti ambao utazuia kabisa rushwa katika nchi
yetu na jambo hili bado serikali ya CCM hailifanyi’.
Chapisha Maoni