HOME
“Nilikuwa
naendesha gari nilipofika eneo la tukio,taa za gari zilimulika sehemu
hiyo ,nikamuona mwanamke akiwa amekabwa shingo na vibaka na walipoona
gari walikimbia kusikojulikana huku wakifanikiwa kumpora Simu,mkoba
pamoja na vinywaji alivyokuwa navyo mkononi”aliongeza.
Kamanda
Kamugisha alitumia fursa hiyo kuvitaka vijiji,vitongoji, kata pamoja
na mitaa kuwa na jeshi la ulinzi shirikishi ambalo husaidia kwa kiasi
kikubwa kuwakamata watuhumiwa kutokana na wahalifu hao kuishi ndani ya
jamii na wanafahamika.
Ndani
ya wiki moja katika manispaa ya Shinyanga kumeripotiwa matukio sita ya
uhalifu ambayo hufanywa na vibaka, kwa kukaba watu na kuwanyang’anya
mali zao na wanaokuwa wagumu kutoa mali basi huambulia kuwajeruhiwa kwa
kuwakata na mapanga katika sehemu mbalimbali za miili yao na kisha
kuwapora kwa nguvu.
Tukio kama hilo limetokea wiki chache ziliopita linamhusu Mwenyekiti wa Halmashauri mpya ya Ushetu mkoani Shinyanga baada ya kuvamiwa na vibaka hao na kuwacharanga mapanga bila huruma pamoja na kuwapora fedha shilingi laki tano na kuwajeruhi vibaya.
SHINYANGA KUMENUKA..!! WANANCHI WAPIGWA MAPANGA BILA HURUMA,WAPORWA KILA KITU
Huyu ni mzee jina tunalo akionesha
majeraha baada ya kucharangwa mapanga na vibaka katika daraja la Mhumbu
barabara ya Shinyanga-Mwanza
Wakazi
wa Shinyanga mjini wameingiwa na hofu kubwa kutokana wimbi la vibaka
kuzagaa katika maeneo mbalimbali wakiwa na mapanga,fimbo na virungu
nyakati za usiku na kukaba,kujeruhi kisha kupora mali za wananchi.
Walisema
tofauti na eneo la daraja la Mhumbu lililoko kata ya Ibadakuli na kule
Ndala katika manispaa ya Shinyanga hivi sasa vibaka wamehamia katika
daraja la Buluba,barabara karibu na Shule ya Sekondari Buluba,eneo la
shule za msingi Bugoyi A na B lakini pia eneo linalozunguka kanisa
katoliki la Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga.
“Inatupa
mashaka sana,tunanyang’anywa simu,pesa na vitu mbalimbali,tunacharangwa
mapanga,tunaomba vyombo vya ulinzi na usalama vitusaidie,haiwezekani
kuanzia saa mbili watu vibaka wajitawale namna hii”,waliongeza wananchi
hao.
Mmoja
wa wananchi hao (jina tunalo)alisema juzi alishuhudia mwanamke akipiga
kelele za kuomba msaada majira ya saa mbili usiku katika maeneo ya
shule ya sekondari Buluba ambapo mwanamke huyo alikuwa amekabwa na
vibaka huku wakiwa na mapanga.
Akizungumza
na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga
kamishina mwandamizi wa polisi Justus Kamugisha alisema jeshi lake
limejipanga vyema kudhibiti vibaka hao na kuwatia nguvuni na kuchukuliwa
hatua kali za kisheria kwani wanahatarisha amani ya wakazi wa manispaa
ya Shinyanga.
Alisema
katika kufanikisha harakati hizo aliwataka wananchi washirikiane na
jeshi hilo kwa kutoa taarifa dhidi ya wahalifu pamoja na maeneo
wanayopendelea kujificha.
“Ndugu
zangu jeshi la polisi haliwezi kufanya kazi peke yake pasipo
kushirikiana na wananchi ambao ndio hufanyiwa vitendo hivyo vya kukabwa
na vibaka na kuporwa mali zao,tunawaomba wananchi kushirikiana nasi,ili
kukomesha wahalifu”,alisisitiza kamanda Kamugisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na malunde1 blog baadhi ya wanachi walisema vitendo vya ukabaji vimekuwa vikifanywa na baadhi ya vijana kuanzia nyakati za saa mbili mjini Shinyanga. |
Tukio kama hilo limetokea wiki chache ziliopita linamhusu Mwenyekiti wa Halmashauri mpya ya Ushetu mkoani Shinyanga baada ya kuvamiwa na vibaka hao na kuwacharanga mapanga bila huruma pamoja na kuwapora fedha shilingi laki tano na kuwajeruhi vibaya.
Chapisha Maoni