HOME
Wafanyakazi
wa Zahanati ya kivukoni, kata ya Minepa,tarafa ya Lupiro wilayani
Ulanga mkoani Morogoro, wamekuwa wakitumia tochi kushona wagonjwa au
kuzalisha wajawazito wanaofika kwa dharura nyakati za usiku, kutokana na
kukosekana umeme au nishati nyingine mbadala ya kuwawezesha kupata
mwanga katika zahanati hiyo.
WAFANYA KAZI WA ZAHANATI YAKIVUKONI HUKO MOROGORO WANAZALISHA WAJAWAZITO NA KUSHONA WAGONJWA HUKU WAKITUMIA TOCHI KUPATA MWANGA
Wakizungumza na ITV katika zahanati hiyo, inayohudumia takribani
wagonjwa 30 kwa siku, wafanyakazi hao wamesema iwapo serikali itatilia
mkazo changamoto hiyo kwa haraka, kuna uwezekano mkubwa wa kusaidia
kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto, sambamba na kuboresha
zaidi utoaji wa huduma, huku wananchi wa kivukoni wakizungumza kwenye
mkutano wa hadhara, wamesema pamoja na kujisajili kwenye mifuko ya afya
ya jamii, bado huduma zinazotolewa katika zahanati hiyo haitoshelezi,
jambo linalowazimu kufuata huduma hizo makao makuu ya tarafa ambako ni
mbali.
Aidha wananchi wameeleza kushangazwa kuona nyumba za watu
zilizojirani na zahanati hiyo zinafungiwa umeme, huku eneo hilo muhimu
kwa jamii likikosa huduma hiyo, ambapo mbunge wa jimbo la Ulanga
magharibi Dk Haji Mponda, amesema tayari serikali imeona changamoto hiyo
na kutenga kiasi cha shilingi milioni saba kufikisha umeme katika
zahanati hiyo na kinachokwamisha hivi sasa ni utaratibu wa malipo ya
serikali.
Chapisha Maoni