HOME
Ziwa Victoria ni ziwa muhimu katika kanda ya Afrika Mashariki,
kati na pia Afrika Kaskazini. Kiuchumi ziwa hilo linategemewa na wakazi
wengi wa eneo hilo kwa shughuli mbalimbali zikiwemo uvuvi, kilimo na pia
usafirishaji. Ziwa hilo la pili kwa ukubwa na lenye maji safi duniani,
hata hivyo linakabiliwa na hatari ya uchafuzi, magugu maji, na kupungua
kwa maji kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani na shughuli
nyingi za binadamu. Mark Muli, mwandishi wetu aliyeko Nairobi, Kenya,
amefuatilia changamoto zinazolikabili Ziwa hili, na jinsi linavyoweza
kunusuriwa kutoka kwa changamoto hizi.
Tarehe 19 mwezi June, ushirika wa ufadhili wa maeneo muhimu ya Ziwa Victoria walizitaka nchi ambazo ziwa hilo linapita au liko karibu kuchukua hatua mwafaka za kunusuru ziwa hili kutokana na changamoto zinazolikabili. Washirika hao ambao wanatoka nchi za Finland, Uswisi, Ujerumani, Japan, Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika, wanasema, pamoja na changamoto nyingi zinazolikabili Ziwa Victoria, serikali za nchi zilizo karibu na ziwa hilo hazifanyi jitihada zozote muhimu kulinusuru na athari hizo. Washirika hao wanaona kuwa, mikakati muhimu inafaa kuwekwa na idara za usalama za kanda hii ili kushugulikia uhifadhi wa ziwa Victoria. Bodi ambayo imepewa kazi ya kushugulikia uhifadhi wa ziwa hili ya Lake Victoria Basin Commission Secretariat - LVBC, inasema kuwa changamoto kubwa katika kazi yake ni kuunda mikakati iliyopendekezwa na nchi husika ili ifanye kazi yake inavyostahili katika uhifadhi wa ziwa hilo. Magugumaji, ambayo ni changamoto kubwa kwa ziwa hili yaliripotiwa katika miaka ya themanini, na mpaka sasa athari za magugu maji hayo hazijakabiliwa kikamilifu. Mmea huu ambao asili yake ni Marekani kusini, una uwezo wa kuenea kwa kasi sana, watafiti wanasema kuwa, kwa wiki mbili mmea huu una uwezo wa kuenea kilomita 50 za mraba, haswa kwenye maeneo yaliyo karibu na makampuni ambako maji yake yanachafuliwa.
Uwepo wa mmea huu katika ziwa Victoria kumeleta taabu sio tu kwa wahifadhi wa ziwa hilo, bali pia kwa wananchi ambao hutumia ziwa hilo kwa shughuli zao za kiuchumi kama vile uvuvi na usafirishaji. Afisa mtafiti katika taasisi ya maswala ya samaki jijini Kampala, Uganda, Dr. Victoria Kibenda, alipohijiwa na Radio China Kimataifa alisema kwamba, ziwa hilo linakabiliwa na changamoto nyingi ambazo kwa sasa zinafaa kushugulikiwa kikamilifu. Akieleza baadhi ya mikakati iliyopo ya kuimarisha hali ya ziwa hili, Dr. Kibenda amesema anaamini kuwa mikakati ikiyowekwa italinusuru ziwa Victoria. Ametaja mikakati hiyo kuwa ni kuanzishwa kwa bodi ya kusimamia mazingira ya Ziwa Victoria, na pia kuanzishwa kwa Shirika la Ziwa Victoria. Dr. Kibenda amesema, vyombo vya habaro pia vinatumika kuwafikia wananchi wa nchi za Afrika Mashariki na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa Ziwa Victoria na samaki wake.
Pamoja na magugu maji, wataalamu wa kisayansi wanasema, changamoto kubwa zaidi kwa ziwa hilo ni uchafuzi unaofanywa na makampuni yanayozunguka maeneo ya karibu. Uchafu mwingi kutoka kwenye viwanda na makampuni yanayozunguka ziwa hili unamwagwa kwenye ziwa hilo, jambo ambalo huchochea kumea kwa magugu maji. Wakaazi wa maeneo ya Dunga, Homabay, Kendubay na nchi nyingine ambazo zinalizunguka ziwa hili wanaeleza kuwa, katika siku za karibuni, uvuvi umekuwa pia changamoto kwa sababu magugu maji ni kikwazo kwa usafiri wa mashua zao wanapokwenda kuvua.
Wafadhili wa shuguli za kumaliza magugu maji na pia watafiti wa kisayansi wanafanya juu chini kupata njia mwafaka za kumaliza magugu maji katika ziwa hilo. Mwezi Machi mwaka huu, Benki ya Dunia ilivikabidhi vikundi vya kijamii vinavyoishi katika maeneo ya karibu na ziwa hilo shilingi milioni 274 ambazo watazitumia kuhifadhi mazingira, hii yote ni katika harakati za kulinusuru ziwa hili. Mikakati mingine ya iliyopo ya kunusuru ziwa hili ni kuwaelimisha wakazi wa maeneo yaliyo karibu na ziwa hili juu ya umuhimu wa kuendelea kuzingatia mazingira bora. Dr. Victoria anasema kuwa, bidii zaidi itaongezwa katika hilo na kwamba, ziwa hili limeanza kurudia hali yake ya zamani kwa kuwahamashisha wanachi na wavuvi kutoka nchi zote za kanda hii kuona umuhimu wa kutunza ziwa hili na maziwa yote, kwani ni raslimali muhimu kwa mwanadamu. Amesema katika kuwahamasisha wananchi, vyombo vya habari vinatumika kuwaelimisha hatari za kuharibu mazingira ya Ziwa hilo.
Kwa ziwa hili kurudia hali ya awali, wadau wote katika setka za utalii, uvuvi, kilimo, na uchukuzi katika kanda ya Afrika mashariki, kati, na kaskazini, wanahitajika kushugulika ipasavyo changamoto zinazolikabili ziwa Victoria.
Ziwa hilo ndio chanzo cha mto Nile, mto ambao ni kiungo muhimu kiuchuni na pia kilimo katika mataifa ya Afrika Kaskazini, kama vile Sudan na Misri. Na kama walivyosema wafadhili wa uhifadhi wa ziwa Victoria, ni sharti mikakati muhimu iwekwe kunusuru ziwa hilo kutoka kwa athari zinazolikumba.1. Haya magugu yapo ndani ya ziwa kama kilometer 3 toka jiji la Kisumu
Hatua zatakiwa kuchukuliwa kulinusuru ziwa Victoria

Chapisha Maoni