Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME JK- Katiba hii nzuri, naomba muipokee Aliyekuwa mwenyekiti wa bunge maalum ...
HOME

JK- Katiba hii nzuri, naomba muipokee


Aliyekuwa mwenyekiti wa bunge maalum la katiba Mh.Samwel Sitta akikabidhi rasimu ya katiba kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS Jakaya Kikwete ameomba wananchi waipokee katiba inayopendekezwa kwa kuwa ni nzuri na hana wasiwasi nayo. “Tumefika mahali pa kuanza safari ya uamuzi wa mwisho kwa kupiga kura.”
Alihadharisha wananchi kwamba wataambiwa mengi kwa kuwa wapo wasemaji wengi. Aliwakumbusha kuzingatia msemo wa akili za mbayu wayu wa kuchanganya akili za kuambiwa na za kwao.
Alisema anaamini Katiba inayopendekezwa inafaa na katiba mpya iliyo nzuri inawezekana.
Alipongeza wajumbe kwa kutendea haki matarajio ya Watanzania na kuwaambia kwamba majina yao yameandikwa kwa dhahabu kwa kutengeneza Katiba inayojumuisha maslahi ya makundi yote na kuyajali. Alitaja makundi hayo kuwa ni pamoja na wafugaji, wakulima, wazee, wanawake.
“Tangu dunia iumbwe, mfugaji hajawahi kutajwa kwenye katiba yoyote ile,” alisema na kuongeza upande wa wanawake kuwa katiba imesisitiza lazima 50 kwa 50 itekelezwe.
Alisema hakuna nchi ya Afrika inayoifikia kwa kuweka suala hilo kwenye katiba. Katiba imependekeza mgawo mzuri wa mamlaka na madaraka katika Muungano. Orodha ya mambo ya muungano ni mpya, yale yote yaliyokuwa yakituletea gozi gozi yameondoka…yamekuwa 16 na siyo 22,” alisema na kusisitiza kwamba mambo yaliyokuwa na kero kubwa upande wa Zanzibari yamepatiwa majawabu.
Alieleza pia kuguswa na uwapo wa sura inayohusu ardhi, maliasili na mazingira ambayo kwa mujibu wake, ndiyo mambo ya msingi ambayo katiba isipokuwa nayo kuna upungufu mkubwa.
Alisema katiba imekubaliwa kwa theluthi mbili kwa kila upande jambo alilosema halikuwa rahisi hasa kwa upande wa Zanzibar ambayo wajumbe siyo wengi.
Tume ya Warioba Rais Kikwete ambaye alipongeza wadau mbalimbali ikiwamo Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba, alisema,
“natambua mengi yamesemwa baada ya tume, katika warsha na makongamano, na mjadala naomba mkumbuke hekima ya wahenga, yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
“ Alisema kila mwenye upande kwenye malumbano hayo, kama ingekuwa ni vita, angesema sasa mapigano yasimamishwe.
Alisema Tume ilitimiza wajibu wake, Bunge la Katiba limemaliza wajibu, kilichobaki ni wananchi kupiga kura. Pia alishukuru vyombo vya habari akisema vimetoa mchango mkubwa wa mawazo kiasi cha mchakato kujulikana kwa wananchi.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top