HOME Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba Waziri Mkuu m...
HOME
Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba
Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu
Katika
mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo
uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku
baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa
ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika
kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa
mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba,
alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Vijana hao ambao haijajulikana
walitokea wapi au walikuwa na ajenda gani waliinua mabango ya kupinga
msimamo wa waliokuwa wakiendesha mdahalo na kusema rasimu ya katiba
iliyopendekezwa inakidhi mahitaji yote na kusema hakuna haja ya mdahalo.
Jaji
Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania alifanikiwa kutoka
nje ya ukumbi ulipokuwa ukifanyika mdahalo huo mjini Dar Es Salaam,
lakini wapo watu waliojeruhiwa kutokana na kurushwa viti na vitu
vingine.
BBC iliwasiliana na Jaji Warioba apate kueleza
yaliyotokea na kama yuko salama baada ya vurugu hizo, lakini aliomba
radhi kwa kusema hayupo tayari kulizungumzia swala hilo.
Kiongozi
wa kitengo cha hamasa umoja wa vijana CCM (UVCCM), Paul Makonda,
aliyekuwepo ukumbini alidaiwa kuhusika na vurugu. Lakini alipoulizwa na
BBC kujibu tuhuma hizo Bw Makonda amekanusha kuhusika nazo huku akisema
kwamba alihudhuria mdahalo kwasababu ulikuwa wazi kwa kila mtu.
Wakati
wa vikao vya Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, Makonda aliwahi kutoa
kauli za kumkebehi Jaji Warioba ambaye tume yake iliandaa rasimu ya
iliyokuwa ikijadiliwa na bunge hilo.
Hata hivyo Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, aliieleza BBC kuwa hana maelezo ya
kutosha na kwamba atalizungumzia akipata taarifa rasmi ya kiofisi.
Tanzania
ipo katika mchakato wa kupata katiba mpya. Rasimu iliyodaliwa na
kupitishwa na bunge lililosusiwa na vyama vya upinzani inatarajiwa
kupigiwa kura na wananchi mwezi Aprili, 2015.
Wachambuzi wa
maswala ya kisiasa wameeleza wasi wasi kuwa endapo hakutakuwa na
kuvumiliana hali ya kisiasa nchini humo inaweza kubadilika na kuleta
ghasia ambazo zinaweza kuepukika.
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Chapisha Maoni