HOME
MWANANCHI
Nimekuwekea hapa mkusanyiko wa Story kubwa tano kutoka kwenye Magazeti ya leo December 25
Kesi ya kuchoma moto bendera ya CCM inayomkabili Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari jana imeahirishwa mpaka January 20, 2015kutokana na Hakimu David Mwita kuwa safarini.
Mbunge huyo pia hakuhudhuria kesi hiyo
kwa kuwa alikuwa safarini, kesi hiyo inatokana na tuhuma anazokabiliwa
nazo za kuchoma bendera ya CCM yenye thamani ya sh. 250,000/- iliyokuwa
mali ya Raphael Moses, yuko huru kwa dhamana ya watu watatu ya sh. Mil.1.5.
MWANANCHI
Hakimu Godfrey Haule wa Mahakama ya Mwanzo Mirerani , Manyara amegoma kumwapisha mshindi wa nafasi ya uenyekiti Mbuki Mollel kwa madai kuwa ushindi wake una utata na kuongeza kuwa atazua mgogoro kwenye jamii.
Hakimu huyo amesema zoezi la kumwapisha
Mwenyekiti huyo litafanyika muda wowote baada ya Mahakama kujiridhisha
na ushindi wa Mollel.
Desemba 14 wakazi wa Kijiji cha Kambia
ya Choka walimsimika Joshua Kuney kuwa mwenyekiti wao wakidai kwenye
kura za maoni CCM ndiye waliyemchagua kwa kura 335 dhidi ya Mollel 215,
huku Mbuki akisema kuwa yeye ndiye Mwenyekiti halali.
NIPASHE
Wajawazito Wilaya ya Chato wameiomba
Serikali Wilayani humo kutunga Sheria ndogondogo za kuwataka wanawake
kujifungulia vituo vya kutolea tiba na kuwabana wanaume kuhudhuria
kliniki ili kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi.
Takwimu za WHO zinaonyesha takribani wajawazito 79,000 hufariki kila mwaka nchini huku kukiwana wastani wa vifo 22 kila siku.
Kumekuwa na mapokeo tofauti kwa wananchi
juu ya elimu ya uzazi wa ampango ambapo wapo wanaoamini kutumia njia za
uzazi wa mpango ni kupingana na agizo la Mungu, wengine wakisema ni
shinikizo la nchi za Ulaya zenye lengo la kurudi kuitawala Afrika na
wengine wakiamini kuwa huo ni mpango kupunguza idadi ya watu kinyume cha
mila na desturi.
Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Chato
amesema Serikali na asasi mbalimbali bado zina jukumu la kutoa elimu
kwa wananchi ili wanadili mtizamo wao kuhusu uzaziwa mpango.
MTANZANIA
Majambazi wamevamia duka na kupora fedha
kiasi cha mil. 4.5 na kumuua kwa kumpiga risasi kichwani Gloria Marandu
maeneo ya Kinondoni, Dar ambaye alikuwa anapita njia.
Kamanda wa Polisi Camillus Wambura
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wahusika wa tukio hilo
hawajakamatwa lakini upelelezi unaendelea.
Wambura amewataka wananchi kutoa taarifa na ushirikiano pale wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.
JAMBO LEO
Ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Kipolisi Tarime, PC Degratias amejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki
ubavuni na wavamiziwa mgodi wa Acacia North Mara walioingia kuokota mawe
ambayo yalidhaniwa kuwa na dhahabu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime, Lazaro
Mambosasa amesema askari huyo alijeruhiwa juzi saa saba mchana
alipokuwa kwenye operesheni ndani ya mgodi huo akiendesha gari ambapo
kundi la watu hao walivamiagarialikyokuwa akiendeshana kumjeruhi.
Askari huyo amelazwa Hospitali ya
Halmashauri ya Tarime akipatiwa matibabu huku Polisi wakiendelea na
upelelezi wa watuhumiwawaliohusika na tukio hilo.
Chapisha Maoni