Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa bomba la
mafuta kutoka Uganda hadi Tanga litakuwa limekamilka kufikia 2020 hivyo
kilichobaki ni kuanza utekelezaji wa kuanza kujenga bomba hilo.
Profesa
Muhongo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na
waandishi wa habari juu ya mikakati walioweka katika kutekeleza ujenzi
wa bomba hilo, amesema kuwa wataalam katika sekta mbalimbali kutoka
Uganda na Tanzania wamekutana leo jijini Dar es Salaam kuweza kuweka
mikakati hiyo ya kuanza kutekeleza bomba hilo.
Muhongo
amesema kuwa kutokana na maagizo ya Rais Dk.John Pombe Magufuli na
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Mseveni ya mradi wa bomba la mafuta
watendaji kazi yao ni kuanza kufanya utekelezaji na wataweza kumaliza
kabla ya mwaka huo baada ya kupata muongozo wa wataalam wataowasilisha
Mei 26 Oima nchini Uganda.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea
uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na mafuta
katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini
Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.
Waziri
huyo amesema kuwa Uganda imetoa asilimia 40 kwa nchi Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuweza kununua hisa hizo ili kuwa na sehemu ya kunufaika na
bomba hilo ikiwa hisa hizo zinauzwa kwa Dola za Kimarekani Bilioni 4.7.
Amesema
kuwa kwa nchi makini haiwezi kuacha kununua hisa hizo kutokana na faida
ya mradi huo na nchi itakayoacha kununua hisa hizo sio makini.
Amesema
bomba hilo lina umuhimu kwa kujengwa nchini ambapo Tanzania itaweza
katika kujenga bomba la gesi kwenda uganda kutokana na uhitaji wa
Waganda wa gesi inayozalishwa nchini.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini
Profesa James Mdoe ( wa kwanza kushoto, waliokaa mbele); Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk.
Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kushoto waliokaa mbele) pamoja na
wataalam wengine wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini
hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini
Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni (hayupo pichani) katika mkutano
kati ya nchi ya Tanzania na Uganda lengo likiwa ni kujadili mpango wa
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi katika bandari ya
Tanga nchini Tanzania.
Naye
Waziri wa Maendeleo ya Nishati na Madini wa Uganda, Mhandisi Irene
Muloni amesema kuwa bomba hilo likijengwa litanufaisha nchi mbili ambazo
ziko katika huo mradi huo na unafanywa na wataalam katika nchi mbili.
Mhandisi
Irene amesema kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi hivyo Uganda
inahitaji gesi ambayo wataipata Tanzania kutokana na mahitaji ya viwanda
nchini humo.
Amesema
vyombo vya habari ni wadau muhimu katika kuhabarisha wananchi wa Uganda
na Tanzania kwa kila kitu kinachoendelea kwa masilahi ya mapana ya kwa
nchi ambazo mradi zinatekeleza.
Wataalam
kutoka Wizara, taasisi na makampuni ya mafuta kutoka Tanzania na Uganda
wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inawasilishwa na mwakilishi
kutoka kampuni ya Total katika mkutano huo.
Aidha
ameipongeza Tanzania katika kuwa sehemu ya watekelezaji wa mradi huo na
kuahidi kuendelea na ushirikiano katika miradi mingine.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Dk.
Fred Kaliisa (kushoto) akifafanua jambo katika kikao hicho. Kulia ni
Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene
Muloni.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.
Kulia ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda,
Mhandisi Irene Muloni.
Waziri
wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni
(kulia) akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kukamilika kwa mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Balozi wa Uganda Nchini Tanzania, Dorothy Hyuha akifafanua jambo katika mkutano huo.
Chapisha Maoni