HOME
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anaongoza mkutano huo
uliowaleta pamoja viongozi 120 , ukiwa ni mkusanyiko mkubwa wa viongozi
wa ngazi ya juu tangu mkutano uliofanyika mjini Copenhagen kuhusu
mabadiliko ya tabia nchi uliomalizika bila kupatikana muafaka mwaka
2009.
Wanadiplomasia na wanaharakati wa mazingira wanaliona tukio hilo kuwa ni muhimu katika kujenga msukumo kabla ya mkutano utakaofanyika mjini Paris baadaye mwaka 2015 ambao utaangalia upatikanaji wa makubaliano ya kupunguza gesi zinazoharibu mazingira baada ya mwaka 2020.
Lakini viongozi wa China hawahudhurii mkutano huo , nchi ambayo ni mtoaji mkubwa wa gesi hizo zinazoharibu mazingira , pamoja na India , nchi iliyoko katika nafasi ya tatu ya kwa uchafuzi wa mazingira, na hii inaweka kiwingu cha shaka kuhusu mafanikio ya mkutano huo.
Hakuna muda wa kupoteza
Mabadiliko ya tabia nchi ni suala muhimu kwa wakati huu, amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
"Najisikia hamasa kubwa kutokana na nguvu na hamasa za sauti za watu. Ni matumaini yangu sauti hizi zitafika kwa viongozi wakati watakapokutana Septemba 23. Mabadiliko ya tabia nchi ni suala muhimu katika wakati huu. Na hakuna muda wa kupoteza."
Ban Ki-moon atazindua mkutano huo akiwa pamoja na makamu wa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati wa mazingira Al-Gore, mcheza sinema maarufu Leonardo DiCaprio, mcheza sinema kutoka China Li Bingbing na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Rajendra Pachauri , mkuu wa jopo la mazingira la Umoja wa Mataifa.
Viongozi baadaye watazungumza mmoja baada ya mwingine, kuanzia rais Barack Obama wa marekani akiwakilisha nchi ya pili duniani kwa utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira hadi waziri mkuu Enele Sopoaga wa taifa la visiwa vya Tuvalu, ambalo linakabiliwa na uwezekano wa kufutika duniani kutokana na kupanda kwa kiwango cha maji ya bahari.
Wanaharakati hawana matumaini hata hivyo
Licha ya hamasa kubwa kutoka kwa wanaharakati wa mazingira kwa uwezo wa mkutano huo kuwa ni kichocheo , baadhi wanauona kuwa unamapungufu ya kile kinachohitajika kuchukua hatua za dhati juu ya mazingira.
Mamia ya waandamanaji walizuwia njia karibu na soko la hisa , katika hatua iliyopewa jina la Wall Street imefurika.
"Madaraka yako mikononi mwa watu hawa wakati watakapo rejea katika mataifa yao na miji na makabila na kuanza kufanya kazi inayokusudiwa. Watakwenda pamoja na Umoja wa Mataifa."
Hatua hiyo imekuja karibu na siku ya kimataifa siku ya Jumapili ya kuchukua hatua na imewaleta pamoja watu wanaokadiriwa kufikia 310,000 katika mitaa ya mjini New York katika kile wanaharakati wanachosema ni maandamano makubwa kabisa kuwahi kufanyika kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
Mkutano wa mazingira kuanza mjini New York leo

Chapisha Maoni