HOME
AJALI YAUA WATU WANNE BAADA YA COASTER KUPASUKA TAIRI NA KUGONGA HIACE HUKO MOSHI
Watu
wanne wamefariki papo hapo na wengine watano wamejeruhiwa katika ajali
ya barabarani iliyotokea leo mchana eneo la Uchira katika barabara kuu
ya Moshi/Dar baada ya bus la kampuni ya kilenga kupasuka tairi na
kuyumba barabarani na kugongana na bus dogo aina ya toyota hiace.
Walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea saa saba mchana wakati
bus hilo aina ya costa lililokuwa likitoka Moshi kwenda Same kugongana
na bus dodo aina ya Toyota hiace ambalo lilikuwa linatoka Moshi kwenda
Mwanga.
Wamesema, dreva wa bus dogo alishindwa kulikwepa bus la kilenga na
kwenda kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu hao waliokuwa
ndani ya Toyota hiace.
Muuguzi wa zamu wa hospitali ya rufaa ya KCMC Bi Justine Haule
amethibitisha kupokea miili ya marehemu wanne akiwemo mwanamke mmoja na
wanaume watatu na majeruhi wanawake wanne na mwanamme mmoja.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Godfrey Kamwela
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na jeshi la polisi linaendelea
kukusanya taarifa na kufanya uchunguzi zaidi na kutoa taarifa kwa umma.
Chapisha Maoni