Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Breaking News!! RAIS KIKWETE AMPIGA CHINI WAZIRI TIBAIJUKA,MUHONGO AWEKWA KIPORO Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jak...
HOME

Breaking News!! RAIS KIKWETE AMPIGA CHINI WAZIRI TIBAIJUKA,MUHONGO AWEKWA KIPORO



Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete 
akihutubia taifa la Tanzania kupitia wazee wa mkoa wa Dar es salaam jioni hii 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Anna Tibaijuka ametenguliwa rasmi nafasi yake ya Uwaziri na Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete amesema wamemueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka kuachia ngazi ili apate kuteua waziri mwingine.

Kuhusu Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Rais Kikwete amesema huyu amemuweka kiporo kwanza maana bado uchunguzi unafanyika.

Rais Kikwete"Waziri wa ardhi Tibaijuka kupokea pesa za Escrow , tumekaa nae na kuzungumza. Pesa hizi ni za nini na kwa ajili gani na amesema ni za shule, mengi yameelezwa. Maswali makubwa kwa nini hazijaenda shuleni moja kwa moja na zikawa kwa jina lake, akasema ndo masharti ya mtoaji, tumelitafakari sana na tumeona msingi mkubwa wa kimaadili kuhusu kupokea hizi pesa, tumeshazungumza nae na tumemwambia atupe nafasi tumteue mwingine.

Waziri Muhongo huyu tumwemweka kiporo,
Waziri wa nishati na madini tumemuweka kiporo, kuna uchunguzi nimeagiza ufanywe na nikipata majibu nitafanya uamuzi, tume ya maadili pia wanafanya kwa ajili ya kupata maamuzi kwa misingi ya haki.
Nitafanya maamuzi siku hizi mbili tatu",Rais Kikwete



Prof. Anna Tibaijuka aliyeng'olewa uwaziri jioni hii nchini Tanzania


Prof. Sospeter Muhongo aliyewekwa kiporo

Nimepita katika ukurasa wa Facebook wa Mwandishi wa habari Dotto Bulendu  yeye ametoa mchanganuo huu  juu ya hotuba ya Rais Kikwete

PESA ZA ESCROW SI ZA UMMA,ASEMA RAISI KIKWETE,
-ANADAI SERIKALI HAIKUPATA HASARA YOYOTE KUTOKANA NA SAKATA HILI,
-ATENGUA UTEUZI WA PROF TIBAIJUKA KWA KUKUBALI KUWEKEWA PESA KWENYE AKAUTI YAKE BINAFSI.
-AMUWEKA KIPORO PROF MUHONGO,WAKATI UCHUNGUZI BADO UNAENDELEA,AKIPATA MAJIBU ATATOA UAMUZI.
-APANGUA BAADHI YA MAPENDEKEZO YA BUNGE.
-ADAI CCM WALIKUWA IMARA KWENYE SAKATA LA ESCROW
-AWATAKA CCM NAO WAKAWAAMBIE WANANCHI KUHUSU ESCROW
-AKIRI KUWA UJAMAA USHAKUFA KITAMBO
,huu ndi mchanganuo wa aliyoyasema raisikkikwete kuhusu ESCROW hii leo.
i) AMEKIRI KUWA TANESCO ILIKUWA INAIBIWA NA IPTL
ii) TRH 5.7.2006 NDIYO ACCOUNT YA TEGETA ILIFUNGULIWA NA KUFIKIA TAMATI TRH 5.9.2013 MAHAKAMA ILIAMURU SHUGHULI ZOTE ZA TANESCO ZIKABIDHIWE KWA IPTL HUKU KUKIWA HAKUNA KESI ILIYOFUNGULIWA ACHILIA MBALI ILE YA MWANZONI YA MALALAMIKO YA TANESCO KUWA WANAIBIWA KUPITIA CAPACITY CHARGE
iii). PESA ZILIKAA KWENYE ACCOUNT YA ESCROW KWA MIAKA 7.
iv) .Wakati CAG anakagua kulikuwa na shilingi 202 Bilioni nukta tisa.
v) Kama Tanesco wangeli tozo za uwekezaji,akaunti hii ingekuwa na shilingi Bilini 306.7,kutokana na Tanesco kutolipa ilibaki na madeniya shilingi Dola Bilioni 33.6 na IPTL.
vi) .Account ya Ecsrow haikuwa na Bilioni 306,bali zilikuwemo Bil 202 pekee ambazo IPTL ilikuwa inaidai Tanesco.
vii).Amesema kuwa kutoka na hali ya mgogoro ulivyokuwa pesa zilizokuwa ndani ya akaunti ya ESCROW SI ZA UMMA BALI NI ZA IPTL kwani ndiyo mlipwaji kutokana na madeni ambayo IPTL inaidai TANESCO kutokana na tozo za uwekezaji.
vii).Kuhusu majibu ya CAG,kuhusu pesa ni za nani?raisi amesema kama Tanesco wangeshinda mgogoro wao na IPTL basi pesa hizo zingekuwa za UMMA kama ilivyokuwa kwenye kesi yao ya mwaka 2001,ila kwa sababu Tanesco walishindwa,pesa hizi ni za IPTL na si UMMA(PUBLIC)
viii),KUHUSU KUWEMO KWA KODI ZA SERIKALI NDANI YA ESCROW ACCOUNT KIASI CHA BILIONI 21 NA MILIONI 700,AMESEMA PAP WALIPELEKEWA DENI LA KODI YA SERIKALI,AMESEMA CAG ALIKAGUA NA KUSEMA PESA ZILIZOKUWEMO KWENYE AKAUNTI YA ESCROW HAZIKUWA NA SIFA ZA KUITWA PESA ZA UMMA.
ix).Trh 15.9.2013 mahakama kuu ya Tanzania ulifanya uamuzi wa maombi ya kampuni ya VIP kuomba kusimamisha mchakato wa kuuza hiza za IPTL wakilumbana juu ya hisa,uamuzi wa mahakama ulikuwa PAP wapewe hisa 30 NA WAKANUNUA HISA 70 na waliandikisha hisa 70 Brela,mahakama ikaamua hisa zikabidhiwe PAP ambao ndiyo mmiliki halali wa IPTL.,Uamuzi huu wa mahakama ulimaanisha kuwa PAP wanatakiwa kumiliki mpaka pesa za ESCROW kwa PAP,umauzi ambao ulizuia malumbano serikalini juu ya akauniti ifungwe ama isifunwe,pesa zitoke ama zisitoke.
x).Wizara ya nishati na madini waliamu kuomba ushauri kwa mwanasheria mkuu juu ya pesa,AG alielekeza kuwa pesa zilipwe kama mahakama ilivyotaka,benki kuu waliuliza maswali haya,na AG akaelekeza walipe kwa PAP na hakuna kodi,ushsuri wa AG uliitoa nafasi ya akaunti kufungwa na kugawanywa rasmi na baadae kuingia barabarani.
xi).Maamuzi yote yaliyofanyika yalifanyika kwa maelekezo ya mwanasheria mkuu,umuzi huu wa mwansheria kuu umeibua mjadala mkuu kuwa kuna rushwa kubwa,watu wamemegewa mshiko,kila mtu kaongea.
xii).Amekanusha kuwa kufungwa kwa akaunti ya ESCROW hakukuwa na msukumo kutoka kwa maafisa wa serikali,amesema serikali ilifanya juhudi kubwa kwenye sakata hili.
xii).Amesema mwanasheria mkuu alimwambia hakukuwa na makosa yeyote kwenye maamuzi ya mahakama,na pia hakuna hasara ambayo serikali imepata kutokana na sakata hili la ECSROW kwa sababu pesa hizo zilikuwa ni deni ambalo Tanesco ilikuwa inadaiwa na IPTL.
xiii).Kuhusu kuwa PAP walinunua hisa za PIPAL LINK huku kikuwa na amri ya mahakama ya kutouza hisa,amesema bado vyombo vya mamlaka vinachunguza

xiv).Kuhusu uuzwaji wa hisa,amesema napo kunahitaji uchunguzi zaidi hasa bei ya hizi hisa.
xv).Amesema Rugemalira alilipa kodi aliyokuwa anadaiwa kiasi cha shilingi Bilioni 38,RUGEMALIRA hana makosa kwenye hili,Alilipa kodi zote.
xvi).KUHUSU MAPENDEKEZO CAG ameelekeza taaifa zile zipelekwe PCCB.
xvii).Kuhusu waliomegemewa pesa na RUGEMALIRA,amesema Takukuru na tume ya maadili ya watumishi wa umma wanachunguza na kushuhulika na watumishi wa umma wote waliopewa pesa,amesema tume ya maadili ya umma itawahoji wote waliopewa pesa.
KUHUSU MAZIMIO YA BUNGE
i.Amesema serikali imeyapokea maazimio na itayafanyia kazi
ii.Kuhusu kutaifisha mitambo ya IPTL,amesema si sawa kutaifisha sababu kutafukuza wawekezaji
iii.Kuhusu uwazi wa mikataba,amesema serikali itafanya mapitio ya mikataba,amesema kuna haja ya serikali na bunge kukaa pamoja na kuzungumza,kwa sababu kuna makampuni yanataka usiri wa mikataba(company secret)
iv)Kuhusu PCCB,na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vichukue hatua,amesema tayari utekelezaji ueanza.
v).Kuhusu kuwavua vyeo wenyevitio wa kamati amesema bunge ndilo litekeleza.
vi).Kuhusu kuundwa kwa tume ya kijaji kuwachunguza majaji waliohusika na sakata la ESCROW,amesema itabidi kuzingatia utaratibu wa kikatiba na sheria,amese suala hili linatakiwa kuanzia kwenye mahakama,halianzii kwa raisi wala bungeni,Amemuachia Jaji mkuu alishughulikie na kumpelekea mapendekezo raisi.
vii).Kuhusu mamlaka husika za kifedha na kiuchunguzi ziitaje Stanbic bank na benk zilizohusika zitangazwe kuwa taasisi zinazotakatisha fedha amesema uchunguzwe na mamlaka husika.
viii).Kuhusu serikali iandae na kuwasilisha marekebisho ya sheria ya uundwaji wa rushwa kubwa,amesema hilo ni wazo zuri,na serikaliimekuwa inaifanyia marekebisho taasisi ya kuzuia rushwa tangia mwaka 2008
ix).Kuhusu kuwavua nafasi zao watumishi wa umma wakiwemo mawaziri waliotajwa,raisi Kikwete amesema,Bodi ya Tanesco imeshamaliza muda wake,hili lishajifuta,kuhusu katibu mkuu Maswi amesema mamlaka zinazohusika zianze ushunguzi wa kuchunguza tuhuma zake,mwanasheria mkuu ameshajiuzulu,kuhusu mawaziri(TIBAIJUKA) amesema wamezungumza nae na wamekubaliana aachie ngazi,kuhusu Prof Muhongo amemuweka kiporo..
NAJIPA MUDA KABLA SIJATIA NENO.
  • Kulwa Makomba NILIJUA TU HUYU MAMA WATAMTOA KAFARA.
  • Iman Julius Imeipenda kias cha pesa bilion 202 na co bilion 306
    39 mins · 1
  • Godlove Nkya Haya sasa Tibaijuka.....rudisha ule mzigo
  • Mapesa Zabron hivi hii nchi inawatu au viatu? kama pesa ilikuwa cyo ya umma kwan tibaijuka alikosa nn kuwekewa kwenye ac yake? hao wazee wamemsikiliza mpaka mwisho hata mmoja wa kujilipua akaokoa taifa
  • Clement Mungure Tezi dume hii ni balaaa
  • Monzo Murasi Doto mimi nilitegemee muhongo atabaki na kwa kweli nimefurahi sana
    37 mins · 1
  • Samwel Bujiku Huyu ndo rais zero kulko wote dunian.kaz kuchekacheka kama shoga.
    36 mins · 1
  • Mapesa Zabron tez jike nayo inakuja
  • Shaban Mputa Ukishakuwa fisadi lazima utafute njia ya kuwalinda mafisad wenzako!! Bunge lilipopendekeza mitambo itaifishwe haikuwa na nia mbaya ni kwa ajili ya kukomesha na kulinda maslahi ya nchi ili wenye nia au wanaodhan Tanzania ni taifa lege lege wasije wakathubutu !! Unapowalinda kwa kuogopa tutaonekaje ni udhaifu wa hali ya juu na kuruhusu kuendelea kufanywa shamba la bibi na wawekezaji..
  • Sophia Hebron jAMANI NIMEUMIA SANA NITA COMMENT KESHO
    32 mins · 1
  • Anselemi John Lugela HII NDIYO TANZANIA BORA INGEKUA TANGANYIKA
    32 mins · 1
  • Mapesa Zabron tz wezi ndo wawekezaji!!! du! hii kali
  • Fedeo Fedeo mimi namuona muhongo kama profesa anayelekea kubaya cjaona kwanini ang'ang'anie kuendelea kuwa chini ya uchunguzi, anapelezwa kwan yeye kibaka? mnaomshauri mwambieni tu asije akaaibika kama mwenzie, taratibu apishe arudi darasani
  • Mathayo Thomas Mwanasiasa mwongo huyo
    24 mins · 1
  • Boniface Myalla Uko safi kaka,
    24 mins · 1
  • Peter Fadhily ivi swala la werema limeisha kienyeji namna hyo??.Inasikitisha sanaaaa.
    24 mins · 1
  • Aloyce Mchunga Tanzania wanamhitaji Jakaya Kikwete kama mhimili wao uliotukuka. Pengine wangemwangalia kama kiumbe tu ingekuwa bora zaidi.
    22 mins · 2
  • Masatu Salum alivyoeleza kama ni kwel nimemwelewa vzur sana na ametumia madaraka yake vzur kumtemesha tibaijuka
    20 mins · 1
  • Edward Mwanicheta Kaka nilikuwa nauvizia UPM
    19 mins · 1
  • Alex Digga CCM mwisho Kikwete kaimaliza Inakuaje Tibaijuka amtolee maamuzi akawaogopa wanaume pigo kubwa linakuja 2015 kuanzia katiba mpaka uchaguzi mkuu mamaaaaaa wamekwisha
    15 mins · 1
  • Christian Kulwa Phillip Ametukana watanzaniaa kwa kutupaa story zisizo Na mpangooooo Na kushangaza zaidi ameacha jembe lake muhongo Na maswi waendelee kula bataaaaaaa wakat watanzania tunakufaaa hospital kwa kukosa dawa..mikopo..Maji
    ..Na matatizo lukuki....umetuhadaha watanzaniaaa
  • Masatu Salum Ulitaka na nani mwngne huku yy amemutoa wazr aliyekura hela vip kwenye majaj kasemaje
  • Masatu Salum Jk hana maamuz magumu kazidiwa na HAWA GHASIA
HAYA NDIYO NIMEYAKUTA UKURASA WA FACEBOOK NA TWEET YA ZITTO KABWE


Mmesikia wananchi?
  • 67 people like this.
  • Rodrick Lyimo Bado mmoja.
  • Allan Moshi Jk kama angekuwa kipa, ni bingwawa kukwepa penalti!
  • Mwanaharakati Kenloo Nimemckia ila cjamuelewa
  • Osward Simon Mim xina cha kusema coz na hasila sana...
  • Tabitha Justine Hahahaha tumesikia weeee
  • Christopher Bunju Eti kiporo alikuwa anafanya maongezi ya nn km hana ushahid wakutosha
  • Rebbecca Siyame Tumesikia bwana.
  • Musa Mtenzi kiporo hicho....
  • Godfrey Mtei tumesikia uchunguzi bado unaendelea
  • Damson Asheri kigugumiza kwa mhongo
  • Amos M. Mafwiri Rais wa ajabu kabisa kuwahi kutokea chini ya jua. Kama huyu Rais hausiki na wizi huu basi ni Juha. Naona aibu kujitambulisha na ninaongozwa na Rais Kimeo kama huyu Jamaa.
    1 hr · 2
  • Matokeo Isaya Wapiiiii maaamaaa tibaijuka? Jembe la kikwete!!!@!@@@
  • Adam Shamba Ni shidaa, nashindwa kuelewa inakuwaje mtu anachunguzwa wakati huohuo anaendelea na kazi..hasa kwa ishu kubwa za tuhuma za rushwa...
    58 mins · 2
  • James M. Yusuph Ha haaaa...!!! Kiporo jamani...
  • Amiry Swaleh namuonea huruma rais wangu jmn dah!
  • Philipo Millanzi duh, tunaish ktk nch ambyo wez wanalindwa ila raia asiye na hatia anauwa na polis wanaojfnya uxalama wa raia, jaman .... ni bora ardh yetu ya Lindi na Mtwara irudishwe Msumbiji tuepukane na haya majanga!!!!
  • Ally Ramadhani Sijui tumelogwa
    57 mins · 1
  • Lucas Mwigani Wkt wa uchunguz mtuhumiwa hutakiwa kupisha ofc ila kwa tz kila kitu ni kawaida
    56 mins · 1
  • Babuu Mkulima Mdogo Nimesikia lakini sijamwelewa hata chembe,, labda mloelewa mnisaidie...
    Katwambia ela n za iptl mwshon anakubaliana na mapendekezo ya bunge yalyojengwa ndan ya msingi wakuwa katka zle pesa iko pesa ya umma!!! Cjaelewa
    Km mwanasheria mkuu kawajbika kwa ushauri wake kutoeleweka hiyo ina maana kuwa hata kodi haikuwepo ktk hiyo pesa ya escrow,,,ht maana ya escrow imefutika,,
  • Vivianeritha Niccolaus Mukebezi Kwa Anna safi tunaomba nawengine wafuate
  • Ignas Karuhawe Kitabu cha mfalme Juha mnakikumbuka mlopita shule? Mi nilsmuliwa tu
    52 mins · 1
  • Ally Ramadhani Kwa asiyeelewa hiyo inaitwa formation ya 4-5-1 
    Mwanasheria unajiuzulu mizigo yooote unatupiwa wewe ili kulinda wengine..... N ileile kama Richmond
  • Adam Shamba Sielewi pia wakati gani rais wetu anakuwa serious...sikupenda hata kidogo kumuona anacheka ktk hotba hii...je ni kweli alikerwa na jambo hili? Yaonekana alimuita tu 'bumkubwa' akamwambia kishkaji 'ishakuwa noma' wakaelewana...
    50 mins · 2
  • Laban Muttamwega Mh.Zitto hili sio la wananchi tu Bali lianzie ndani ya Bunge ......ilitakiwa wasitoke pale ndani na kwakua mliruhusu hilo basi JK sawa.
  • Elsante Eljouf JK na Washikaji
    46 mins · 1
  • Viva William Mmmmmh Nilidhani mambo magumu yaaani Rais kaongea kwa wepesi sana.
    45 mins · 1
  • Mogela Makonga otumesikia ila bado tunamaswali meeengi kichwani...mfano kama account ya escrow ilikua kwaajili ya malipo kwa iptl kabla ya mahakama kutoa uamuzi wa kuifunga bado malipo tulikua hayajafanywa , kulikua na mgogoro ...sasaa kwa wakati huo pesa ilikua mali ya nani?
    iweje maamuzi yatoke kabla ya suluhisho? hakuna rushwa hapa?
    OK... vp kuhusu kuhusu kodi ya serikali nani alizembea au hakutimiza wajibu wake..amechukuliwa hatua gani?
    iptl iliwezaje kuendelea kutoa huduma kwa zaidi ya miaka saba bila kulipwa na Tanesco? 
    Mwanasheria mkuu anachukuliwa hatua gani zaidi kwa ushauri mbovu unaitia hasara taifa?
    #ZittoZkabwe
  • Emanuel Goodluck Kant naona mizengwe tu eti pesa c zauma..mmmh he cant be serious
  • Khalifan Ally Mlambalazi Nakumbuka maneno yako kaka(Mungu hamtupi mtu mwenye dhamira ya kweli hawezi shindwa hawezi kata tamaa) hivyo akae akijua atawalinda hatachoka ila sisi hatutachoka milele mpaka mwisho wa maisha yetu kwa ajili ya UTANZANIA wetu.
  • Yossima Sitta Its not fear
  • Alinanuswe Maclean nitakuwa mtu wa mwisho kumkubali JK, kuna haja ya kumng'oa kwa nguvu ya UMMA
  • Stigger Kidulla KIKWETE NI KIONGOZI SHEITWANI ANALINDA MASHEITWANI WENZAKE, TUPO NYUMA YAKO MH Zitto Z Kabwe
  • Aziz Salehe 2014 ctausahau kwa vituko shoo
  • Raymond Julius Sawa kaka tumesikia matusi haya
  • Emmanuel E. Meela Rais ni mnafiki sijawahi ona. Yaani anapenda funza wa chooni lakini anachukia kinyesi. Kwa mliosoma kitabu cha "Things fall apart" cha Chinua Achebe watanielewa. Haiwezekani akubaliane na mapendekezo ya Bunge then hapo hapo awatetee baadhi ya wezi. Unafiki ulioje.!!!!
  • John Steph Mwayahila chenge vipi sjaskia akitajwa
  • Kashaigiri Richard Lengo lake mahususi lilikuwa kumlinda Waziri mkuu. Manake kama angetamka kuwa ni pesa za umma moja kwa moja Pinda angetakiwa kujitathini kwa kupingana na rais wake. Anyway,,, not so bad.
    21 mins · 1
  • Back Stage That the way they wanted to play it...kama mama tibaijijuka angejiuzulu leo raisi angeonekana hajafanya kitu nd dat the reason hata tibaijuka akafanya press conference...they fake us...!! Everythng is fake...!!
  • Bernad Mwambagi Loading.......
  • Rugzy AndreJr Haikuwa hotuba ilikuwa ni msela anaongea na wasela wenzie
  • Agness Isowe Tumesikia maana hata hakieleweki huyu profesa kweli maamuzi magumu kwake yeye ni mepesi

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top