HOME
MWANANCHI
Mkusanyiko wa Stori kubwa kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 9, 2015 Nimekuwekea hapa
MWANANCHI
Polisi wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JNIA wanamshikilia raia wa Kuwait kwa tuhuma za kukutwa na kenge 149 kati yao 139 wakiwa hai, akidaiwa kutaka kuwasafirisha.
Kamanda wa Polisi JNIA, Suleiman Khamis alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Hussain Ahmed na alikamatwa juzi usiku akijiandaa kuelekea kwao Kuwait kupitia Dubai akitumia ndege ya Shirika la Emirates.
Alisema mtuhumiwa huyo alitumia mifuko midogo ya rambo kuwahifadhi kenge hao na kuwaweka ndani ya begi kubwa jeusi.
“Kila
mfuko ulikua na kenge 15 na kati yao 15 walikua wamekufa na wakati
tunafanya upekuzi ndipo tulipogundua kuna vitu visivyo vya kawaida
mithili ya nyoka ndani ya begi lake na tukaamua kuwashirikisha watu wa
maliasili na kubaini kuwa ni viumbe hai aina ya Kenge,”alisema Kamanda Suleiman.
Mtuhumiwa huyo kwa sasa anaendelea kuhojiwa na mara baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
MWANANCHI
Mfumuko wa bei kwa mwaka uliomalizika
umeshuka hadi kufikia asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.8 kutokana na
kupungua kwa bei za bidhaa mbalimbali ikielezwa kuwa kupungua huko
kulikua hakujawi kutokea kwa miaka miwili mfululizo.
Mkurugenzi wa sensa za watu na Takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alisema kushuka huko kunatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji bei ya bidhaa na huduma ikilinganishwa na ilivyokua Novemba.
Alisema mfumuko wa bei za vyakula na
vinywaji umepungua hadi asilimia 5.7 Desemba kutoka asilimia saba ya
mwezi uliokua umetangulia.
Alitaja baadhi ya vyakula vilivyochangia
kushusha mfumuko huo kuwa ni pamoja na mahindi yaliyoshuka kwa asilimua
11.3, unga wa mahindi 7.6, samaki 4.0, ndizi za kupika 3.2, mbogamboga
11.5, muhogo 10.5 na sukari iliyoshuka kwa asilimia 4.2.
NIPASHE
Askari wa kituo kikuu cha Shinyanga
aliyefahamika kwa jina moja la Alex,amewekwa korokoroni akituhumiwa
kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkazi wa kata ya Ngokolo na
kumsababishia maumivu makali sehemu zake za siri.
Kamanda wa Polisi Shinyanga, Justus Kamugisha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli kamili.
“Tunaendelea
kufanya uchunguzi lakini sina haja ya kutaja jina lake kwa sasa hadi
tutakapokamilisha upelelezi wetu na kujiridhisha,”– Kamugisha.
Mama mdogo wa mwanafunzi huyo akisimulia
mkasa huo alisema mwanaye alitoka usiku kwenda kujisaidia na ndipo
alipokutana na askari huyo ambaye alimvutia chumbani kwake kisha
kutekeleza unyama huo.
MTANZANIA
Afya za Watanzania zipo hatarini baada
ya kuingizwa kwa sukari inayodaiwa kuwa feki ambayo imekua ikisambaa
mitaani kwa kutumia vifungashio vinavyoonyeshwa inazalishwa na kampuni
ya sukari ya Kilombero.
Mwenyekiti wa Chama cha wakulima cha Msindazi, Ayubu Mora alisema sukari inatoka nchi jirani ya Uganda na kwa kiasi kikubwa inauzwa kwenye maduka makubwa.
“Hii
sukari inatoka Uganda na inaingia nchini na kuuzwa kwenye maduka na
kuwekwa nembo ya Kilombero,kiwanda cha hapa hakitengenezi sukari nyeupe
lakini zipo madukani,hii inahatarisha maisha ya Watanzania kwa kiasi
kikubwa,hatuko salama“– Ayubu.
Akijibu suala hilo Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kamati yake inafuatilia kwa ukaribu suala hilo na wameiagiza TRA kufanya uchunguzi na kubaini kiasi cha fedha ambazo Serikali inakosa kutokana ukwepaji wa kulipa kodi hiyo.
MTANZANIA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda
amesema yeye si kiongozi wa kulialia jambo linalomfanya ashindwe kutoa
maamuzi mbalimbali ya Serikali kama watu wengine wanavyodai.
Pinda alisema kumekuwa na baadhi ya watu wanaobeza uwezo wake wa utendaji kazi jambo ambalo yeye anapingana nalo.
“Kumekua
na watu ambao wanabeza mimi sifai kuwa kiongozi kwa vile nashindwa
kutoa maamuzi mbalimbali katika mambo yanayohusu Serikali na ninapokua
Bungeni eti nalia“– Pinda.
Alisema uvumi huo hauna ukweli juu ya utendaji wake wa kazi kwani amekuwa akitoa uamuzi pale ambapo anahitajika kufanya hivyo.
“Nataka
Watanzania wanielewe,nimekua nikitoa uamuzi mwingi wa bila kutangaza
kwenye vyombo vya habari,huwa sipendi kufanya hivyo kwa kuwa si kila
jambo lazima litangazwe“– Pinda.
HABARILEO
Imeelezwa kuwa zaidi ya asilimia 70 ya Watanzania,sawa na watu milioni 31.5 wapo hatarini kupata magonjwa ya ngozi kutokana na kutumia vipodozi visivyo sahihi.
Kutokana na hali hiyo imesisitizwa ipo
haja ya elimu ya athari za vipodozi kutolewa kuanzia shule za msingi
kwani wengi wanaoathirika wanakua na uelewa mdogo juu ya matumizi sahihi
ya vipodozi.
Daktari bingwa wa magonjwa ya ngozi katika hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi, Eliafoi Masenga alisema kutokana na uelewa mdogo Watanzania wengi wanaathirika na amekuwa akitibu wagonjwa wa ngozi 12,000 kwa mwaka.
“Zaidi
ya asilimua 70 ya watu wanatumia vipodozi visivyo sahihi na wengi wao
wanaathirika kutokana na uelewa mdogo,ni vyema elimu itolewe kuanzia
ngazi ya shule za msingi“– Masenga.
Alitaja baadhi ya dawa za hospitali zinazouzwa katika maduka ya dawa za vipodozi kuwa ni lemovate, clobetasol, betacort, diproson na mediven.
Alisema sheria inaeleza wazi kuwa
anayeuza vipodozi haruhusiwi kuuza dawa za hospitali na aliye na dawa za
hospitali haruhusiwi kuuza vipodozi visivyo na sumu lakini lakini watu
wamekua wakikiuka sheria hiyo.
HABARILEO
Hofu imetanda juu ya Masheikh jijini
Kampala Uganda baada ya wenzao wanne kudaiwa kutekwa na watu
wasiojulikana na kupelekwa mafichoni.
Hayo yamethibitishwa na Katibu wa Jumuiya ya Tabligh Uganda, Ayub Nyende akisema ni kweli wametekwa na kwamba juhusi za kuwatafuta karibu maeneo yote ikiwemo vituo vya Polisi zinaelekea kukwama.
“Mazingira
ya kutoweka kwao hayajulikani na hakuna mwenye majibu mpaka
sasa,tumechanganyikiwa kwa sababu hakuna dalili ya wao kupatikana“– Nyende.
HABARILEO
Mradi wa ujenzi wa bomba la gesi asilia
utaleta manufaa makubwa kwa Taifa na wananchi wake ikiwemo utekelezaji
wa dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2015 na utasaidia kuokoa shilingi
trilioni 1.6 kwa mwaka.
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maendeleo la Petrol nchini TPDC ikilenga
kuelekeza utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia kutoka
Madimba-Mtwara, Songosongo-Lindi na Pwani hadi Dar es salaam, imetaja
manufaa mengi ya kiuchumi ya mradi huo.
Kwa mujibu wa mradi huo utawezesha
upatikanaji wa umeme wa uhakika na bei nafuu jambo ambalo litasaidia
kuokoa zaidi ya trilioni 1.6 kwa mwaka.
Fedha hizo zitatumika sasa kuagiza mafuta kwa ajili ya kufua umeme kwa kutumia mitambo ambayo ipo chini.
UHURU
Serikali kupitia wakala wa umeme vijijini REA imetumia bilioni 881 kutekeleza awamu ya pili ya mradi wa kusambaza umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo alisema mradi wa pili utasaidia vijiji vilivyounganishwa na umeme kufikia 3,734 kati ya 15,180 ambayo ni sawa na asilimia 24.6.
Alisema awamu hiyo iliyoanza mwaka 2013
lengo ni kuhakikisha vijiji vyote Tanzania vinapatiwa umeme ili
kuboresha masiha ya Watanzania na kukuza uchumi wa nchi.
Alisema pia Serikali itatumia bilioni 25.7 kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 170 vilivyondani ya Mkoa wa Simiyu.
Chapisha Maoni