HOME
MWANANCHI
Wakati utata ukizidi kujitokeza katika uapishaji wa viongozi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Dar es salaam kutokana na waliodaiwa kushinda kuwekwa kando na kuapishwa walioshindwa,Naibu wa Kazi na ajira Makongoro Mahanga jana alikumbana na zomeazomea hadi kulazimika kuondoka kwenuye ofisi za Manispaa ya Ilala ambako shughuli hiyo ilikua ikifanyika.
Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Segerea kupitia CCM alizomewa akitakiwa kuondoka katika eneo hilo,akidaiwa kwamba angebadilisha matokeo na kuwapa ushindi wagombea wa Chama chake.
Eneo hilo lilijaa wafuasi wa Chadema,CUF na CCM huku kila kundi likiwa limesindikiza wenyeviti wake kuapishwa katika shughuli ambayo ilifanyika kwa awamu tatu kwa kila jimbo,Segerea,Ilala na Ukonga kupewa saa mbili.
Waziri Mahanga aliwasili wakati wa zamu ya Segerea saa 7:oo mchana,ndipo kundi la mashabiki wa upinzani lilipoanza kumzomea na kuimba nyimbo za kumkashifu na kutaka atoke ndani ya ukumbi huo ulioandaliwa kwa ajili ya kuapishwa.
MWANANCHI
Wakati mjadala wa bei ya mafuta ukiendelea,imebainika kuwa bei ya nishati hiyo nchini ni kubwa ukilinganisha na ya Kenya,wakati Rwanda ikiongoza kwa kutonufaika kwa kushuka kwa petrol katika soko la dunia kati ya nchi za Afrika Mashariki.
Mafuta yameporomoka bei kutika soko la dunia kutoka dola 115 za Marekani hadi chini ya dola 50 kwa pipa tangu Juni 2014.
Takwimu zinaonyesha kuwa Wizara zote zinazoshughulikia mafuta,isipokua Uganda,zimepunguza bei kwa viwango tofauti.
Wakati Rwanda,Burundi na Uganda hazina bahari,Kenya na Tanzania zinapakana na bahari ya Hindi na hivyo kutoathiriwa sana na gharama za usafirishaji.
Lakini petrol nchini Kenya ilipungua bei tangu Desemba 15 na kuuzwa kwa sh.1,719.7,wakati bei iliyoanza kutumika nchini ni sh.1,955.
MWANANCHI
Sakata la ufisadi wa zaidi ya bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow limewang’oa wafanyakazi saba wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.
Wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa maazimio manne ya Bunge kuhusu ripoti ya kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC kuhusu kashfa hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alisema pia Serikali imetoa siku 30 kwa walionufaika na mgawo wa mamilioni ya fedha kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya VIP Engeneering ltd,James Rugemarila kulipa kodi kulingana na kiasi walichopewa.
“Mpaka sasa wafanyakazi saba wamesimamishwa ili kupisha vyombo vinavyohusika viweze kuchukua hatua kwa kuwa haiwezekani badala ya dola milioni 20 mtu anaweka fedha za Tanzania sh.20 milioni,hii ni makusudi ama njama za kutekeleza wizi huo”alisema Nchemba.
NIPASHE
Naibu Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba amesema makundi mbalimbali ya kijamii yamemuomba agombee urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.
Nchemba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM alitaja makundi hayo kuwa ni pamoja na viongozi wa dini za kiislam na kikristo,wanafunzi wa vyuo vikuu,Watanzania wanaoishi nje ya nchi,wakulima na watu wanaoishi vijiweni.
Hata hivyo Mwigilu alipotakiwa kutoa kauli yake kama atagombea,hakutaka kukubali wala kukataa na badala yake aliwashukuru wake wote waliokua wakimtumia ujumbe kumtaka agombee.
Mwigulu alisema atatoa maamuzi yake ya kugombea ama la kipenga kitakapopulizwa akimaanisha muda rasmi CCM itakapotangaza kuanza mchakato wa uteuzi wa wagombea.
MTANZANIA
Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limeendelea kuwakamata vijana wanaodaiwa kuhusika na vitendo vya uhalifu maarufu kwa jina la Panya Road.
Watuhumiwa 329 zaidi wametiwa mbaroni jana katika operesheni katika Mikoa miwili ya Kipolisi Ilala na Temeke na kufanya idadi yao kufikia 953.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki alisema maeneo mengi ambayo vijana wengi wamekamatwa ni kwenye vijiwe wanapohusika na uvutaji wa bangi,dawa za kulevya na uvutaji wa pombe haramu aina ya gongo.
“Vijana hawa hawana dhamana kwa sababu ndio chimbuko la Panya road wanaohatarisha amani kwa wananchi ambao wanashindwa kufanya kazi zao kwa uhuru na amani,”alisema kamanda Nzuki.
MTANZANIA
Tatizo la ugonjwa wa moyo kwa watoto linazidi kushika kasi baada ya Mikoa ya kanda ya Ziwa kuonekana iko hatarini zaidi.
Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Hospitali ya rufaa ya Bugando,Dk Neema Kiyange alisema watoto wanaofanyiwa uchunguzi hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa mwaka jana ,300 wamekutwa na ugonjwa huo.
Alisema wazazi na walezi huchelewa kuwapeleka watoto wao kwa ajili ya uchunguzi wakidhani wamerogwa na kujikuta wakikimbilia kwa waganga wa kienyeji.
MWANANCHI
Mtoto wa miaka 12 mkazi wa Mkoa wa Geita ametimuliwa nyumbani na mama yake mzazi na kutakiwa kwenda kuishi maisha ya kujitegemea baada ya kuunguza mboga jikoni.
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya Msingi Karangalala ameamuriwa na mama yake kufanya hivyo baada ya mama yake Helena kumwachia jukumu la kupika mboga Novemba mwaka jana lakini mboga hiyo iliungua.
Baada ya kuunguza mboga hiyo,mama huyo alimpiga mwanaye kabla ya kumpa masurufia na kumkabidhi chumba tayari kwa kuanza maisha.
Mtoto huyo alisema mama yake amekua na tabia ya kumpiga mara kwa mara kiasi cha kusababisha mwili wake kuwa na alama za viboko.
“Sifahamu kwa nini mama yangu huwa ananipiga kiasi hiki,inawezekana kwa kuwa na yeye alilelewa na mama wa kambo aliyekua anampiga hivi”alisema mtoto huyo.
HABARILEO
Watu wanne wakazi wa Wilaya ya Iramba,wakiwemo watumishi wawili wa Halmashauri ya Wilaya hiyo wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kufanya jaribio kutaka kumuua Mkurugenzi wa Wilaya kwa kutumia bomu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Thobias Sedoyeka amethibitisha na kusema watu hao wamehifadhiwa kutokana na kutokukamilika kwa uchunguzi na walikamatwa kwa nyakati na maeneo tofauti.
Sedoyeka alisema ujumbe ambao Mkurugenzi huyo alitumiwa umekwishapelekwa kwa mtaalam wa kung’amua miandiko ili kuweza kugundua mtu aliyeandika.
Alisema Mkurugenzi huyo ambaye mwezi uliopita alinusurika kifo baada ya kiyu kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka kitandani mwake.
JAMBOLEO
Chama cha Tanzania Labour Party TLP kimevurugwa kutokana na Katibu mkuu wake,Jeremiah Nchanjala kujiuzulu nafasi yake kwa madai ya kutotendewa haki na kutoshirikishwa katika baadhi ya mambo ndani ya chama.
Katibu huyo alisema hawezi kuendelea kufanya kazi sehemu ambayo hakuna maendeleo kama ilivyo ndani ya TLP na kwamba amechukua uamuzi huo Disemba 15 na kumuandikia barua Mwenyekiti wake Augustino Mrema kwenda kwa msajili wa nyama vya siasa.
“Nimeona niachie nafasi yangu pamoja na kujiuzulu uanachama na nimemwandikia barua Mwenyekiti na nakala itaenda kwa msajili wa nyama,kimsingi nimechukua maamuzi bila kushurutishwa au kushauriwa na mtu yoyote”alisema Nchanjala.
Mkusanyiko wa Story 8 kubwa zilizopewa uzito kwenye Magazeti ya leo Tanzania January 8, 2015

Chapisha Maoni