HOME
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waandaaji:
East Africa Business and Media Training Institute (EABMTI) kwa kushirikiana na TWAWEZA Tanzania wanatarajia kuzindua mijadala ya wananchi katika ngazi za Mikoa ili kutoa fursa kwa wananchi hao kujadili maeneo muhimu wanayotaka yaongoze mijadala ya kampeni za uchaguzi 2015. Mijadala hii inalenga kuwarudisha wananchi katika kutafakari kwa makini juu ya nini wanachokitaka wakati huu nchi inapoelekea kwenye uchaguzi.
Kumekuwa na mijadala mingi sana kitaifa kuhusu Tanzania tunayoitaka, mingi sana ikiishia hewani ama kuhodhiwa na watu wachache au makundi ya watu. Hakujawa na fursa za kutosha za kuwawezesha wananchi kujipanga na kujiwekea vipaumbele. Ni kwa sababu hii EABMTI na TWAWEZA imeandaa midahalo katika mikoa ya Mbeya, Arusha na Mwanza ili kutoa nafasi kwa wananchi hao kuweka vipaumbele vya kile wale wanayotaka yazungumzwe wakati wa kampeni za uongozi.
Wananchi wa maeneo mbali mbali wana vipaumbele tofauti. Fursa hii itawapa wananchi hao nafasi ya kujitazama na kujiwekea vigezo vikiwemo sifa za kiongozi wa eneo lao wanaomtaka wao, mambo wanayotaka na namna wanavyotaka kuongozwa ili kufikia ile Tanzania Wanayoitaka.
Washirikiki:
Mijadala hii inatarajia kuhusisha washiriki wote toka eneo husika wakiwemo wawakilishi wa wananchi, ofisi za wakurugenzi za Halmashauri husika, Asasi za kiraia, wafanyabiashara, makundi maalumu wakiwemo wakinamama, walemavu
Wazungumzaji:
Wazungumzaji wakuuu wanatarajiwa kutoka ofisi za Halmashauri, vyama vya wafanyabiashara , wawakilishi wa asasi zisizo za kiserikali, makundi maalum.
Muongozaji:
Mijadala yote hii itaongozwa na muanzilishi na muongozaji wa vipindi vya Mdahalo vya Tanzania Tunayoitaka.
Mijadala hii itasikika kupitia Radio za mikoa ya Mbeya, Arusha na Mwanza. Vipindi maalumu vitafuatia kurushwa kupitia vipindi maalumu.
Imetolewa na
Ms Alawiya
Coordinator

Chapisha Maoni