HOME
Umewahi kukutana na usafirishaji wa magendo kwa njia hii?
Jamaa
mmoja aliyekuwa akitokea China kwenda Hong Kong ametiwa nguvuni kwa
kosa la kusafirisha simu kwa njia ya magendo, huenda kilichomponza ni
namna alivyokuwa akitembea.
Watu walimshangaa kutokana alivyokuwa
akitembea, wakawashtua maafisa wa Usalama, wakamfuatilia mtu huyo ili
kujua sababu ya yeye kutembea hivyo.
Jamaa huyo alionekana akitembea kama
amezidiwa na kitu kizito, alionekana akiwa amebeba mifuko miwili ya
plastiki lakini isingemfanya aelemewe kiasi hicho, alipofika kwenye
mashine zilizokuwa kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya ukaguzi zilipiga
kelele na alipokaguliwa alikutwa na simu 94 za iPhone 5 na 6 alizokuwa
amezifunga kwenye tumbo, mikono na miguu yake kwa gundi.
Simu hizo zilizuiwa huku Maofisa wa Usalama wakiendelea na upelelezi juu ya tukio hilo.
Chapisha Maoni