Unknown Unknown Author
Title: KUTOKA BUNGENI: GESI KUTUMIKA KUKOMESHA MAUAJI YA VIKONGWE
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME DODOMA MBUNGE wa Viti Maalum Faida Mohamed Bakari (CCM), ameitaka Serikali kupeleka nishati ya gesi vijijini ili kukomesha maua...
HOME
DODOMA

MBUNGE wa Viti Maalum Faida Mohamed Bakari (CCM), ameitaka Serikali kupeleka nishati ya gesi vijijini ili kukomesha mauaji ya vikongwe wenye macho mekundu yanayotokana na kupikia kuni au kinyesi cha ng’ombe.

Alisema hayo bungeni jana wakati akiuliza swali la nyongeza akihoji ni lini serikali itawasaidia wazee hao kwa kuwapelekea gesi kwa ajili ya kupikia ili kuweza kuyanusuru maisha yao.bungeeeeAlihoji “Watu wanawaua wazee na wanawafukia wakiwa hai eti ni washirikiana kisa wana macho mekundu, je, serikali itawasaidiaje wazee hao wa kuwapelekea gesi ili wasiuawe na itikadi za kishirikina?”.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Yussuf Masauni, alisema serikali imechukua mikakati mbalimbali kuhakikisha matumizi ya kuni na kinyesi cha ng’ombe kwa ajili ya kupikia yanapungua kwa kuanzisha majiko sanifu na hata usambazaji umeme vijijini.

Alisema tangu Julai mwaka jana hadi Machi mwaka huu jumla ya watuhumiwa 135 wamekamatwa na kesi 222 zinaendelea mahakamani na serikali inawadhibiti wananchi wote ambao wamekuwa wakijichukukia sheria mikononi.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top