HOME
Chaguzi za Meya wa Jiji la Dar es salaam ziliahirishwa mara tatu na baadaye akapatikana Diwani wa Kata ya Vijibweni, Temeke Isaya Mwita ‘Chadema’ kuwa shauku kubwa ilihamia kwenye kumjua atakayekuwa naibu wake.
April 21 2016 umefanyika uchaguzi wa
Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam ambapo wajumbe 16 kati 18 walifika
kwa ajili kushiriki uchaguzi huo. Matokeo ya uchaguzi yalimpa ushindi
Diwani wa kata ya Kiwalani Musa Kafana ‘CUF’ ambapo alishinda kwa kura 10 na kumshinda mpinzani wake Diwani wa kata ya Mchafukoge Mariam Mohamed ‘CCM‘ aliyepata kura 6.
Kwa matokeo hayo Mussa Kafana ‘CUF’ ndiye amekuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es salaam
Chapisha Maoni