Unknown Unknown Author
Title: PAPA WEMBA ATAKUMBUKWA KWA KIPI?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME   Hivi karibuni tasnia ya muziki wa Dansi iliingia katika majonzi baada ya kumpoteza nguli wa muziki wa Dansi kutoka Jamhuri...
HOME

Image00004 

Hivi karibuni tasnia ya muziki wa Dansi iliingia katika majonzi baada ya kumpoteza nguli wa muziki wa Dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, aliyekuwa akifanya shughuli zake za muziki hapa nchini Ndanda Kosovo.

Wadau wa muziki huo wakiwa katika hatua za kusahau kwa kilicho tokea kwa Ndanda Kosovo, Mwenyezi Mungu anaamua kumuita gwiji mwingine wa muziki huo Papa Wemba kwa staili ile ya Vivian Foe ambaye yeye alianguka uwanjani huku Papa Wemba akianguka ghafla jukwaani.Image00002Taarifa za kifo cha staa huyo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 66 zimewashtua wengi kwani wadau wa muziki wa dansi walipenda kuendelea kuuona mchango wa gwiji huyo, ambaye alianguka ghafla akiwa jukwaani kwenye tamasha la FEMUA linalo endelea Abijan nchini Ivory Coast.

Je Papa Wemba atakumbukwa kwa kipi?, katika maisha ya mwanadamu kuna mazuri na mabaya hivyo moja ya mambo ambayo wadau wa muziki wa dansi watazidi kumkumbuka Papa Wemba ni umahiri wake wa uimbaji na matumizi ya kiswahili katika tungo zake.Image00003

Bendi kama Zaiko Langalanga na Viva la Musica zilifaidika na uwepo wa Papa Wemba katika bendi hizo za nchini Congo, halikadhalika nyimbo zake Yoleyole na Show Me zitabaki kwenye mioyo ya wadau wa muziki wa dansi.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top