Unknown Unknown Author
Title: WAUZAJI WA DAWA BARIDI WAPIGWA MSASA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME Na Martha Magawa Imeelezwa kuwa watu wengi wamekuwa na tabia ya kujichagulia dawa za kutumia kabla ya kupima afya zao hali i...
HOME

Na Martha Magawa

Duka-la-Dawa-BaridiImeelezwa kuwa watu wengi wamekuwa na tabia ya kujichagulia dawa za kutumia kabla ya kupima afya zao hali inayowapa ugumu wamiliki wa maduka ya dawa nchini.

Akizungumza na mtembezi.com mmoja kati ya wamiliki wa maduka hayo, Israel Mwakilasi amesema kuwa tabia hiyo inayofanywa na baadhi ya wateja imetajwa kuwa chanzo cha wamiliki wa maduka ya dawa kukiuka maadili ya kazi zao  kutokana na ubishi wa baadhi ya wanunuzi.

“Wateja wengi wamekuwa ving’ang’anizi wanataka wapewe dawa wanazotaka wao hata kama haziruhusiwi kwa matumizi ya binadamu hasa kwa watoto”. Alisema Mwakilasi

Kwa kuliona hilo Chama cha Wafamasia Nchini (PST) wameamua kufanya mkutano na wauzaji na wa maduka ya dawa za binadamu Jijini Dar es Salaam ili kuongeza ujuzi kwa wamiliki na wauzaji wa maduka hayo.

Nelson Faustine ni Mhazini wa Chama cha Wafamasia Tanzania ambapo amesema lengo la mkutano huo ni kuhamasisha jinsi ya kuhifadhi dawa za kuzuia kuharisha pamoja na nimonia kwani ndio magonjwa hatarishi kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top