Habari na Picha za Freddy Macha, London
Nembo iliyopendekezwa...
Jumamosi
Mchana 7 Aprili ilikuwa siku ya jua kali Uingereza. Wananchi wengi
walijazana bustanini au sehemu za starehe wakiota jua na kula barafu za
sukari yaani "Ice Cream." Magari yalipiga honi, wenyeji waliheushwa na
ujoto ujoto huu adimu mazingira ya Ulaya. Ndani ya ofisi ya Ubalozi wa
Tanzania London, kundi la Watanzania wanane lilikaa mchana wote
likijadili (kwa ari na mori) maslahi ya wananchi wenzao Uingereza.
Chini ya uenyekiti wa Bi Mariam Kilumanga Kikosi Kazi (Task Force – UK,
juu pichani) kilichoundwa na Balozi wa zamani Uingereza Mhe Peter
Kallaghe, kabla hajamaliza wakati wake hakikulegeza kamba. Mazungumzo
makali yaliangalia kuhusu katiba mpya yrnyr kurasa 16. Itafanyiwa
marekebisho kusimamia Jumuiya Mpya ya Watanzania Uingereza. Moja ya
matumaini yake ni kuunganisha na kuendeleza maisha ya wananchi wetu
nje ili kuwafaidi wao na walioko nyumbani. Hebu tazama picha na video
uone taswira ilivyokuwa...
Mwenyekiti Mariam Kilumanga, akihimiza jambo. Bi. Kilumanga ni pia
mwenyekiti wa muda mrefu wa Chama cha Kina Mama Watanzania Uingereza ,
TAWA. Anaipenda sana nchi, dada huyu.
Michael Semuguruka, mkazi wa LondoN Mashariki, ni kati ya wajumbe 12 wanaojitolea wakati wao kwa shughuli hii. ...
Katibu Mkuu, Cleopa John (kulia) na mjumbe Respigy Peter Michael ndani ya kikao. Akili zinazotoa cheche.
Jane
Ngereza, Mmoja wa wajumbe na kati ya wanawake watano ndani ya kikosi
hiki kisichotaka kubabaisha watu. Alisafiri toka Birmingham kuhudhuria
kikao London.
Daniel Semwenda, mjumbe asiyecheka cheka ovyo, akichangia hoja.
Vijana
, Said Surur na Renatus Mgetta, wenye bidii, nidhamu, uzalendo na azma
ya kuunganisha Watanzania. Uzalendo kitu adimu simu siku hizi Afrika.
Taswira
ya Ubalozi wa Tanzania, mtaa wa Bond Street, katikati ya London.
Ubalozi ulimlipa mlinzi wake, fedha za OVATAIM, kuwasubiri wazalendo
hawa kuumiza vichwa.
WAJUMBE AMBAO HAWAKUWEPO KATIKA KIKAO
- Raymond Binya
- Henry Kimani
- Brian Ngerangera
- Jackson Msuku
- Sabrina Karim
- Lucile Shigikile
- Peter Gabagambi
- Jane Kimani
- Amos Msanjila - Afisa Balozi , mhusika, aliyekuwepo halafu akaendelea na shughuli nyingine za Ubalozini.
SIKILIZA UFAFANUZI ZAIDI
https://youtu.be/P76coQOLM98
Katibu...
https://youtu.be/izA1IWHWeuI
Naibu Mwenyekiti...
https://youtu.be/Y_0Po4Inp4o
Katibu Mwenezi...
https://youtu.be/U3OwiI3_K-I
Mjadala mkali kutafuta ufafanuzi haklka wa Katiba
Chapisha Maoni