HOME
BRN Hoi Shinyanga_WANAFUNZI WAJISAIDIA PORINI,WAKALIA MAGOGO,MWALIMU MKUU ATAJWA KWA UZEMBE
BRN Hoi Shinyanga_WANAFUNZI WAJISAIDIA PORINI,WAKALIA MAGOGO,MWALIMU MKUU ATAJWA KWA UZEMBE
Hiki ni choo kinachotumia na wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Mawemilu iliyopo kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga
Ndani ya darasa la tatu katika shule ya msingi Mawemilu iliyopo kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga
WANAFUNZI wanaosoma katika
shule ya msingi Mawemilu iliyopo kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya
ya Shinyanga wanajisaidia vichakani
kutokana na ukosefu wa vyoo vya kutosha , huku
walimu wakilazimika kwenda kutumia vyoo vya
familia ya walimu ambazo ziko jirani na shule hiyo hali ambayo inaweza
kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Moja ya darasa lililopo katika shule ya msingi Mawemilu kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,likiwa halina hata dawati mmoja wanafunzi wake wanakalia magogo ya miti na mawe. |
Hali hiyo ilibainika jana
baada ya waandishi wa habari kutembelea shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 511 na walimu 11 na
kujionea hali halisi ,huku vinyesi vikiwa vimetapakaa nje vya vyoo viwili
vilivyoezwa kwa nyasi ambavyo vinatumika
kwa sasa pia havikidhi mahitajikutokana na idadi ya wanafunzi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Joseph
Chagaka akizungumza na waandishi wa habari alikiri kuwepo kwa changamoto
hizo huku akisema awali kulikuwepo na matundu ya vyoo sita
kwa wanafunzi, lakini yalititia kutokana na mvua za masika zilizokuwa
zikinyesha na kwamba upande wa vyoo vya
walimu hakuna hivyo kufanya kazi katika mazingira magumu.
.
“Tunachangamoto kubwa katika shule hii,
tuliamua kujenga choo hicho chenye matundu mawili kwa kutumia nyasi ili wanafunzi
watumie kwa muda tukiwa tunaendelea kujipanga na ujenzi mwingine wa
kudumu,nina amini havitoshelezi kukidhi mahitaji kwani kuna wanafunzi 511 ,kwa ujumla hali siyo
nzuri tunahitaji serikali itusaidie’’alisema Chagaka.
Hiki ni choo cha wanafunzi ambacho kimeezekwa kwa nyasi kinamatundu mawili na kinatumiwa na wanafunzi zaidi ya 500 wa shule hiyo. |
Mwalimu mkuu wa shule hiyo alisema madawati yaliyopo ni 50 ambayo hayatoshi hivyo kusababisha robo
tatu ya wanafunzi kukaa kwenye magogo na wengine kutumia mawe.
Kwa upande wake afisa
mtendaji wa kijiji hicho Ezekiel Deusi alisema changamoto
kubwa shuleni hapo ni vyoo kwani miundombinu yake ni mibovu ni sawa na hakuna
vyoo , vilivyokuwepo vilititia kipindi cha mvua za masika na sasa wanahitaji matundu 11 ili kuondoa
changamoto hiyo .
Hata hivyo afisa
elimu msingi Andrew Mitumba wa halmashauri hiyo alisema kuwa
kero hiyo ni ya muda mrefu kwani mwalimu
mkuu wa shule hiyo alikwisha
andikiwa barua ya onyo kutokana na uzembe.
“Huu ni uzembe wa
viongozi na serikali ya kijiji, isitoshe
kuna fedha za ruzuku hutolewa kwa shule za msingi ambazo anatakiwa
achukue kidogo na kuanzisha ujenzi na kuchangisha michango kwa wananchi , ili halmashauri
iweze kukamilisha kwa kuezeka maboma lakini huyu mwalimu mkuu hafanyi
hivyo kama alivyoelekezwa,pia suala la ukosefu wa madawati tayari
watapatiwa muda si mrefu
Source:Kadama Malunde na Stella Homolwa
Chapisha Maoni