HOME
HATARI..!! BIBI AJITENGENEZEA JENEZA ILI AKIFA AZIKWE NALO HUKO SONGEA
Mkazi
mmoja wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa
Ruvuma,Bibi Scholastica Mhagama amesema miaka mingi ameishi maisha ya
dhiki na kunyanyaswa bila msaada kutoka kwa jamii anayoishi hali ambayo
imemfanya amuombe Mungu amchukuwe ili azikwe kwenye jeneza
alilojiandalia.
“Kila
siku naomba Mwenyezi Mungu anichukue haraka ili nikapumzike kutokana na
mateso ninayoyapata, lakini hofu yangu nikifa je, nitazikwa kama
binadamu wengine? Ndiyo maana nimeamua kujitayarishia jeneza langu,” anasema Scholastica Mhagama (76) mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
“Nimetengeneza
kabisa jeneza langu siku nikifa wanizike humu. Naomba Mungu anichukue
haraka ili kuepukana na mateso haya. Nimetengwa na jamii na majirani
wanashindwa kunisaidia wanadai eti mimi ni mchawi kwa sababu watoto
wangu wote wanne walikufa wakiwa wadogo. Naumia sana kusingiziwa kitu
ambacho sikijui,’’anasema kwa masikitiko.
Bibi huyo anasema kuwa aliweza kutengeza jeneza hilo baada ya kupewa Sh40,000 na mfadhili mmoja.
“Tayari nilikuwa na mbao kwangu, hivyo kazi ilikuwa kumlipa kijana fedha na kumpa mbao ili anitengenezee jeneza,” anasema
Chanzo cha habari Willium Bundala
Chapisha Maoni