Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME SERIKALI WILAYANI KAHAMA YAFUTA VIBALI VYA UTAFITI KATIKA MACHIMBO MADOGO YA NYANGARATA. Na Shija Felician Kahama ...
HOME

SERIKALI WILAYANI KAHAMA YAFUTA VIBALI VYA UTAFITI KATIKA MACHIMBO MADOGO YA NYANGARATA.


Na Shija Felician
Kahama

Serikali imefuta vibali vya utafiti wa madini ya dhahabu katika maeneo ya Nyangarata na Mwime vilivyokuwa vikimilikiwa na Kampuni za African barrack Gold Mine na Pangea minerals
 
Hayo yameelezwa mjini Kahama na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson mpensya mda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza cha ugawaji wa viwanja vya madini wilayani Kahama
 
Mkuu huyo wa wilaya amesema kufutwa kwa vibali hivyo ni utekelezaji wa mpango wa serikali wa kuwapatia maeneo ya kuchimba wachimbaji wadogo wadogo ambapo sasa machimbo ya Nyangarata na Mwime watagawanywa wachimbaji hao
 
Mpesya alisema kufuatia hali hiyo serikali imeunda kamati ya wilaya itayosimamia ugawaji wa viwanja vya uchimbaji katika maeneo hayo ya Nyangarata na Mwime na wale watakaohitaji watatangaziwa rasmi utaratibu wa kuomba maeneo hayo
 
Kwa upande wake kamishina msaidizi wa madini kanda ya Shinyanga Humphrey Mubando amesema eneo la Nyangarata litagawiwa wachimbaji hao kwa utaratibu wa kamati ingawa lile  la Mwime litagawiwa kwa utaratibu wa kawaida na tayari vikundi vinne vya ushirika vimeomba kupewa viwanja katika machimbo hayo

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top