HOME
SHIRIKA LA SHDEPHA+ TAWI LA KAHAMA LAMUOMBA RAIS KIKWETE AWANYANGANG'ANYE RASIMU YA KATIBA WABUNGE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.
Shirika la Shdepha + Tawi
la kahama mkoani Shinyanga limemuomba rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Jakaya Kikwete awanyang’anye rasmu ya katiba wabunge wa bunge
maalumu la katiba baada ya kubaini zoezi hilo kutekwa na wanasiasa
kinyume na matarajio ya wananchi
Kauli hiyo imetolewa juzi na jana mkoani Shinyanga na mkurugenzi wa shirika hilo Venance Mzuka kwenye kata za Tinde na Kambarange wakati wa mdahalo wa wanawake juu ya rasmu ya pili ya katiba
Katika
mdahalo huo Mzuka amesema lengo la rais lilikuwa na tija kwa
kuwashirikisha wanasiasa lakini badala yake wameenda kufuata maelekezo
ya msimamo wa vyama vyao badala ya maoni ya wananchi hali ambayo hakuna
katiba itakayopatikana kwa masilahi ya watanzania wote
Ili
kumaliza tatizo hilo na kuwatendea haki watanzania wote ni bora rais
sasa akawanyang’anya wanasiasa hao na kulivunja bunge la katiba kisha
akaweka utaratibu mpya utakaowashirikisha wananchi kuanzia ngazi ya kata
Wilaya na hatimaye kuitimishwa na wataalamu ngazi ya taifa
Ushauli
huo uliungwa mkono na washiriki wa midahalo hiyo ambao wameonyesha
kutoridhika na marumbano ya kimasilahi kwenye vyama vya siasa
yanayoendelea na kuongeza kuwa pamoja na msimamo wa serikali mbili ama
tatu unaoendelea lakini wananchi hawajaelezwa kwa kina manufaa ya miundo
hiyo kwa watanzania
Chapisha Maoni