RIPOTI:JESHI LA POLISI LAONGOZA KWA RUSHWA KWA 94% WANASIASA WAPILI KWA 91%.
Jeshi
la Polisi nchini limetajwa kuongoza kwa vitendo vya rushwa kwa asilimia
94 likifuatiwa na wanasiasa wanaongoza kwa asilimia 91 huku msisitizo
ukitolewa kufanya ukaguzi wa gharama za uchaguzi kuanzia ngazi za ubunge
hadi Urais.
Kwa
mujibu wa Utafiti uliofanywa na Shirika la Twaweza umebaini kuwa
asilimia 60 ya wananchi wanaokutana na polisi uombwa rushwa na asilimia
43
ya wananchi hao utoa rushwa kwa polisi.
Twaweza
inasema wananchi watatu kati ya watano wanadaiwa kuombwa rushwa
walipokutana na Polisi na hivyo kuiona rushwa kwenye sekta zote za
serikali kama kitu cha kawaida.
Sekta
nyingine ni afya ambayo ina asilimia 82 wakati kwenye sekta ya kodi
ikiwa na asilimia 80, Ardhi asilimia 79, Sekta ya Elimu asilimia 70,
Serikali za mitaa asilimia 68 na sekta ya maji asilimia 50 huku
mashirika yasiyo ya kiserikali yakiwa na asilimia 50.
Takukuru
inasema wananchi bado hawana uelewa wa mahali pa
kushitaki pindi wanapoombwa rushwa huku Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu kikibaisha kuwa bado hakuna usalama wa kutosha kwa wanaonyesha
nia ya mapambano hayo.
Chapisha Maoni