Wakatazwa kuingia ndegeni, kisa HIV
15 Agosti, 2014 - Saa 14:32 GMT
Abiria wawili wa china waliokuwa
wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la China (China Airline),
wameamua kulipeleka shirika hilo mahakamani kwa kile walichokieleza
kuwazuia kusafiri na shirika hilo eti tu kwasababu walikua wanaishi na
virusi vya ukimwi HIV.
Hata hivyo inaelezwa kwamba abiria hao si mara
ya kwanza kusafiri na China Airline kutoka kaskazini mwa mji wa Shenyang
katika kipindi cha machipuko ,wakati huu sasa shirika hilo la ndege
lilipoamua kughairisha safari za abiria hao.Masharti ambayo abiria hao wameyatoa Kufuatia kughairishwa kwa safari hiyo,shirika hilo la ndege litalazimika kuomba radhi na kulipa fidia ya dola za kimarekani elfu nane .Mahakama katika mji wa Shenyang imeipokea na kukubali kesi hiyo ya kwanza na ya kipekee nchini China.
Viongozi wa serikali kutoka China wamesema kua wamejitahidi kujaribu kupunguza historia ya muda mrefu ya unyanyapaa kwa wanaoishi na virusi vya HIV na ukimwi.
Chapisha Maoni