Unknown Unknown Author
Title:
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOME   Itikadi ya utaifa inavyowagawa wanadamu   MIONGONI mwa itikadi potofu zianzowapoteza waja wa Mwenyezi Mungu na kuwatia utumwani,...
HOME
 Itikadi ya utaifa inavyowagawa wanadamu  
MIONGONI mwa itikadi potofu zianzowapoteza waja wa Mwenyezi Mungu na kuwatia utumwani, katika minyororo ya walimwengu wenzao ni Utaifa. Utaifa ni suala lililowashughulisha walimwengu na kutia uadui baina ya walimwengu. Mwarabu ajiona bora kuliko Mzungu, na Mzungu hujihisi ni mbora kuliko Mwafrika. Mtanzania hujiona tofauti na Mkenya na kama hivi. Utaifa ni nini?
UTAIFA ni dhana iliyoanzishwa maelfu ya miaka. Jean-Jaques Rousseau Mfaransa, ni miongoni mwa mawakala wakuu wa uanzilishi wa dhana hii. Katika maelezo ya Rousseau utaifa ni mahaba ya umoja na mashikamano wa ummah juu ya mapenzi ya nchi ya uzawa. Dhana ya utaifa inapinga imani za dini na muungano wa watu katika dini. Yaani watu washikamane kwa sababu ya uzawa si kwa sababu ya imani ya dini. Mfumo wa utaifa ulisimikwa na mapinduzi ya Ufaransa (French Revolution) ambapo kwanza utaifa ulitekelezwa kwa kivitendo.
Mshikamano huu, umeambatana na mapenzi ya nchi, bendera, kutukuzwa kwa mashujaa na kutungwa wimbo wa taifa. Aidha, utaifa unang'ang'aniza mapenzi juu ya lugha ya wazawa, ubora wa wazawa juu ya waja wengine na imani kuwa taifa lao ndilo teule, lenye haki ya kuongoza, kutafsiri na kuelekeza maadili na kulea walimwengu.
Napoleon Bonaparte (wa Ufaransa) alikuwa miongoni mwa watu waliozidisha hamasa ya utaifa na fikra za Uhuru na Demokrasi. Alikuwa wa kwanza kuieneza mbegu ya utaifa nje ya Ufaransa. Thomas Jefferson na Thomas Paine ndio waanzilishi wa utaifa huko Marekani. Jeremy Bentham aliupa utaifa sura mpya huko Uingereza, Mazzini akausambaza Italia Otto Bisamark huko Ujerumani.
Imani ya utaifa ilipata nafasi ya kuotesha mizizi katika nchi za maghaibi baada ya kutokea ukame wa itikadi. Dini ya Kikristo ilikuwa ndiyo itikadi inayotawala, bali ikavia kutokana na kukosa kwake mwongozo katika nyanja za maisha.
Mkristo alidumaa kuanzia karne ya 17 kwa kukosa ukweli, kutokubaliana na usahihi wa sayansi na teknolojia na kudanganya kwingi. Watu wengi walikosa mwongozo wa maisha nao Ukristo ukabaki makanisani kwa wazee na watu wasiotaalamika. Hapo ndipo utaifa ukapata mwanya wa kuchipuka.
Utaifa uliposhamiri, ukawa ndio baba wa ukoloni. Francis Cooker anatuambia: "Katika karne ya 19 wataifa wengi kutokana na hamasa ya utaifa, waliamini na kudai kuwa nchi zilizoendelea (kiviwanda) zilikuwa na historia ya ufahari na utamaduni bora, na ustaarabu, kwa hiyo hazikuwa na haki ya kufanya uchoyo bali kueneza uwezo na sifa hizo nje ya mipaka yake...". Fikra hizi zilipelekea mataifa kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na kadhalika kukaa Berlin miaka 1884-1885 ili kujadili namna ya kugawana nchi za Afrika na kuzitawala ili ati kuzistaarabisha.
Joseph Lihgten anaandika: "Historia nzima ya karne ya 19 imesimikwa juu ya misingi ya utaifa wa kiuchumi na siasa ambapo utaifa ndio mzizi wa siasa za upanuzi na ugomvi baina ya serikali mbalimbali. William Gladstone (Mwingereza) ndiye aliyeanzisha nchi za dunia ya tatu chini ya bendera ya utaifa, Robert Clive akachochea ukoloni wa Kiingereza huko India, Cecil John Rhodes akavamia kusini mwa Afrika - yakapatikana makoloni ya Northern na Southern Rhodesia.
Hata hivyo utaifa pia si itikadi yenye mwelekeo wa kuongoza watu katika maisha, kwa hiyo huko Afrika Kusini akina Rhodes iliwapasa wachanganye utaifa na dini. Ndipo likazaliwa Kanisa la The Dutch Reformed Church of South Africa lenye sera inayosisitiza kuwa watu wa rangi mbalimbali wasichanganyike. Wazungu peke yao, Waasia pekee, Waafrika peke yao. Kwingineko utaifa wa Kijerumani, Kiingereza na Kifaransa ulidhalilisha ludha, desturi, mila na ustaarabu wa wenyeji ukasimika ustaarabu wao wa kigeni na dini isio na uhai (Ukristo) ili visaidiane.
Katika karne ya 20 utaifa umetumika kuwazingua waliotiwa katika minyororo ya ukoloni na kuanza kudai uhuru. Zilianzishwa sera kama zile za Negritude (Uafrika) na mataifa mapya yakazaliwa na mwana wa halali wa utaifa ukoloni (bali ukoloni pia ulizaa mwana haramu uhuru na demokrasia). Mara baada ya utaifa wa makoloni kuzaliwa, utaifa mama (wa nchi za magharibi) ulizaa ukoloni mamboleo, ubepari na ubeberu.
Kwa ufupi utaifa ni itikadi yenye imani potofu, itikadi isiyotokana na vigezo vya akili bali hisia. Hayawani wote hujitambua wao kwa umbile na silka yao na hawaoni sababu kwanini hayawani wote wasiwe kama wao.
Kundi la nyati hutaka kubaki peke yake, simba, tembo, nguruwe, nyang'au kadhalika. Utaifa imeshereheshwa kwa ndimi za watu ambao aidha hawakukomaa kiakili na busara. Ndiyo maana katika ujahili Mchagga huwaita wasio Wachagga "viasaka". Mpare huwaita wasio Wapare "Wanyika" na kila kundi kama hayawani lilijiona bora kuliko jingine, na lilibagua kundi lingine. Utaifa ni unyama uliopevuka kuliko ule wa hayawani wa vichakani na mwituni.

About Author

Advertisement

Chapisha Maoni

 
Top