HOME
Nchi inahitaji kiongozi mwenye mwelekeo na utambuzi wa dhati kiuelewa namna ya kuleta ukombozi wa haraka katika taifa hili. Nani atafanya hili? Nani mwenye uwezo wa kupigania haki za wanyonge na kusimama kwa ajili ya walio wengi?
Tumefika hapa kwa sababu tulipokea mambo mazito bila kujiandaa, hayati Mwalimu Julius Nyerere hakukubali haya, yalijaribiwa akayakataa, lakini jambo la kusikitisha baada ya kuondoka madarakani, tulipokea mfumo wa uchumi wa kibepari na utandawazi ambao umeendelea kumnyonya maskini hadi kesho.
Miaka ya 1980 hadi 1990, yalikuja mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani ambayo yalitoa msukumo mkubwa wa kuanzishwa kwake kimabavu kwa kulazimisha nchi masikini ikiwemo Tanzania zikubali.
Kipindi hiki kilitawaliwa na mikakati ya maendeleo iliyoongozwa na Benki ya Dunia na Taasisi ya Fedha ya Kimataifa katika kurekebisha uchumi.
Malengo makuu ya urekebishaji huu yalilenga; kulegeza masharti ya biashara, kupunguza nafasi ya serikali katika kusimamia uchumi na rasilimali za taifa, kuweka kipaumbele kwa uwezeshaji wa sekta binafsi, kuondokana na siasa na itikadi ya ujamaa na kujitegemea na kukumbatia upepari na uliberali mamboleo.
Mabadiliko haya yalikuwa na taathira nyingi hasi nchini, zikiwamo kupunguza wafanyakazi hasa kwenye mashirika ya umma, kubinafsisha rasilimali za umma zilizojengwa kwa jasho la wengi ambazo walikabidhiwa wachache.
Wachache waliokabidhiwa mali za umma walikuwa ni wageni kutoka nje waliopewa jina la wawekezaji ambao walianza ubepari wao uliosababisha kujengeka kwa kasi kwa tabaka la wenye nacho na wasionacho.
Majukumu ya huduma za kijamii yalirudishwa katika ngazi ya familia mzigo ambao umeendelea kubebwa na wanawake kwa kiwango kikubwa hadi hii leo.
Kwa sasa kulikuwapo na athari nyingi zinazowakuta wananchi maskini ambazo ni kukosekana kwa huduma muhimu za afya, elimu na miundombinu.
Athari za mfumo huu ni nyingi sana na kwa bahati mbaya zimechangia kuzorota kwa uwajibikaji, kushamiri kwa rushwa, ufisadi na kila aina ya dhuluma inayofanywa na watu waliokabidhiwa dhamana ya kusimamia mali au ofisi za umma.
Ukatili dhidi ya wanawake na watoto nao sasa umezidi kushamiri huku hatua stahiki dhidi ya wanaoutenda zikisuasua.
Kuna uporaji mkubwa wa ardhi, madini na rasilimali mbalimbali ambazo mpaka sasa zinamfanya mwananchi aishi kinyonge na kwenye mazingira magumu.
Kutokana na kukithiri kwa uwajibikaji mbovu, mporomoko wa maadili katika jamii, mashirika yanayotetea haki na usawa wa kijinsia yalianzishwa.
Mojawapo ni TGNP Mtandao, ambalo mwaka huu limeadhimisha miaka 20 ya kuanzishwa kwake na harakati za kudai haki na usawa wa kijinsia.
Mtandao ulijengwa katika misingi ya kupambana na mfumo wa uliberali mamboleo (utandawazi ) na mfumo dume ambayo ndiyo kiini cha tabaka tofauti za kijinsia kati ya wanawake na wanaume zilizochangia kusukuma makundi mengi pembezoni.
Katika muktadha huu wa ujenzi wa kitabaka uliojengeka katika mifumo mingine kandamizi ukiwamo mfumo dume, fursa ya kuanzishwa kwa mtandao huu iliyoelekeza wakati wa maandalizi ya wanawake wa Tanzania kushiriki mkutano wa Beijing mwaka 1995.
Semina tatu za maandalizi ziliongozwa na timu ya wanaharakati kujengeana uwezo. Dhana ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi na mbinu za uraghabishi katika kuibua masuala na wanawake na kuyaainisha katika muktadha wa soko huria na mfumo dume ulitoa hamasa ya kipekee na madai ya umuhimu wa kuanzishwa kwake itakayoendeleza kutandaa na kupashana habari kuhusu masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia na haki ya jamii nchini.
Lengo la kuanzishwa liliongozwa na dira ambayo ni kuona jamii ya Kitanzania inayojali na kuhakikisha haki za wanawake, usawa wa kijinsia na haki za kijamii. Dhima na dhamira yake ni kuwa chachu ya ujenzi wa tapo la ukombozi wa wanawake kimapinduzi.
Hii ina maana kwamba mabadiliko tunayotaka katika mifumo kandamizi na sera zake hayawezi kutokana na vitendo vya mtu mmoja wala taasisi au kikundi kimoja bali tunahitaji kujenga nguvu za pamoja.
Ni lazima kuunghanisha nguvu kwa pamoja ili kushinda vita dhidi ya ukoloni na uporaji wa rasilimali zetu. Hii ni vita inayohitaji mapambano makali ya wengi.
TGNP Mtandao na mashirika mengine wadau wa harakati hizi kwa miaka 20 wametoa mchango wa kipekee nchini Tanzania, barani Afrika na kwingineko duniani, taasisi hii pia imetukuka katika kuwa na msimamo usiotikisika kuhusu umuhimu wa kubomoa mifumo yote kandamizi ili kufikia maendelo endelevu kwa kizazi cha sasa na vijavyo.
Msingi wa dhana ya ukombozi wa wanawake kimapinduzi ni uhusiano wa kijinsia na tabaka, hatuwezi kutenganisha bali tunaunganisha masuala haya kwa maana nia yao ni kubomoa mifumo ya ubepari ubeberu kwa maneno mengine ‘utandawazi wizi’ na mfumo dume.
Kubomoa mifumo vipi? Wao wanaamini kuwa vuguvugu la ukombozi wa wanawake litaongozwa na wanawake walioko pembezoni wanaokandamizwa zaidi kwa kushirikiana na wanaume walioamua.
Ili kushinda vita hii ni lazima kutoka nje na kupaaza sauti, na kusema ‘hatutaki hili na tunataka lile’. Kushiriki katika harakati katika ngazi ya kimataifa kwa mfano, katika miaka ya 2000 wanaharakati wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika walipinga sera za Benki ya Dunia kwa kuunga mkono nguvu za ‘Fifty years is Enough’ (Miaka 50 inatosha).
Kuunganisha kampeni za kidunia na mifumo ndani ya nchi kwa mfano mwaka 2004 kuandamana kupinga mkutano wa viongozi wa nchi 8 za Afrika pamoja na viongozi wa Benki ya Dunia na IMF kidunia (G 8) jijini Dar es Saalaam wakati huo uongozi mkuu wa serikali ukiunga mkono juhudi hizi kwa kutambua kuwa mapambano haya ni ya kukomboa serikali zetu kutokana na makucha ya mfumo wa uonevu wa kidunia.
Tunahitaji ukombozi wa ubepari, ukoloni mamboleo
NCHI yetu inapita katika kipindi kigumu cha kiuchumi na kisiasa. Ni kipindi ambacho kila mmoja amekata tamaa, wananchi wanaoishi vijijini wamekosa tumaini. Tabaka kati ya mwenye nacho na asiye nacho linaongezeka kila siku.Nchi inahitaji kiongozi mwenye mwelekeo na utambuzi wa dhati kiuelewa namna ya kuleta ukombozi wa haraka katika taifa hili. Nani atafanya hili? Nani mwenye uwezo wa kupigania haki za wanyonge na kusimama kwa ajili ya walio wengi?

Chapisha Maoni